Pages

Wednesday, December 30, 2020

RAIS WA ZANZIBAR DK HUSSEIN ALI MWINYI AWATUNUKIA SHAHADA WAHITIMU WA SUZA

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA) Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akihutubia wakati wa hafla ya Mahafali ya 16 ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) katika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein Tunguu Wilaya ya Kati Unguja leo 30-12-2020.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi ametawazwa kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Ndg. Mwita Mgeni Mwita na (kulia kwa Rais) Makamu Mkuu wa Chuo Dkt.Zakia Mohamed Abubakar, hafla hiyo imefanyika wakati wa Mahafali ya 16 ya SUZA yaliofanyika katika ukumbi wa Dk.Ali Mohamed Shein Tunguu Wilaya ya Kati Unguja leo30/12/2020.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi, akimtunuku Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa Katika Sayansi za Tiba Rais Mstaaf wa Zanzibar Awamu ya Saba Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, katika Mahafali ya 16 ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) yaliofanyika katika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein Tunguu leo 30-12-2020.(Picha na Ikulu)

WAHITIMU wa Shahada ya Uzamili ya Sayansi ya Kemia wakitunukiwa Shahada ya Uzamili na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) wakati wa hafla ya Mahafali ya 16 ya SUZA yaliofanyika katika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein Tunguu Wilaya ya Kati Unguja leo.(Picha na Ikulu) WAHITIMU wa Shahada ya Uzamili ya Sayansi ya Usimamizi wa Mali ya Asili na Mabadiliko ya Tabia Nchi  wakitunukiwa Shahada yao na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) wakati wa mahafali ya 16 ya SUZA yaliofanyika katika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein Tunguu Wilaya ya Kati Unguja.(Picha na Ikulu)WAHITIMU wa Shahada ya Usimamizi wa wa Teknolojia ya Habari wakishangilia wakati wa kutunukiwa Shahada yao na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA ) ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) wakati wa hafla ya Mahafali ya 16 ya SUZA yaliofanyika katika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein Tunguu Wilaya ya Kati Unguja.(Picha na Ikulu)

 

No comments:

Post a Comment