Mwakilishi wa Katibu Mkuu,Wizara ya Afya na Mkurugenzi Msaidizi wa Tiba Asili/Mbadala Dkt. Paul Mhame akifungua kikao kazi cha usambazaji wa miongozo inayosimamia huduma za tiba kwa Waganga Wakuu wa Mikoa,Wataalamu wa Maabara ngazi ya Mikoa na Wilaya nchini kwenye ukumbi wa Chimwaga jijini Dodoma.
Mkuu wa huduma za maabara nchini
kutoka Wizara ya Afya Peter Torokaa akiwasilisha miongozo kwa washiriki
wa kikao kazi hicho.Jumla ya miongozo 20 imesambazwa .
Picha ya pamoja ya mgeni rasmi na watumishi wa Wizara ya afya,Mabaraza ya kitaaluma pamoja na Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii
Washiriki wa kikao kazi cha usambazaji wa miongozo
inayosimamia huduma za tiba wakifuatilia ufunguzi ambapo walisisitizwa
kuhakikisha kwamba miongozo hiyo inatumika kwa ufasaha
Washiriki wa kikao kazi hicho ambacho kimehudhuriwa na watendaji katika ngazi ya Taasisi/
Hospitali za Taifa, Mkoa na
Halmashauri pamoja na wawakilishi wa Timu za usimamizi huduma ngazi ya
Mkoa na Wilaya takriban washiriki 300
********************************************
Na. Catherine Sungura,WAMJW-Dodoma
Wataalam wa Maabara nchini
wametakiwa kuongeza kasi katika kuhakikisha huduma za tiba inayotolewa
inafuata miongozi ya wizara na kuhakikisha wanabadili fikra na mitazamo
ili kuwafanya wateja wao waweze kuvutiwa na huduma wanazozisimamia.
Hayo yamesemwa leo na Mwakilishi
wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi wa Tiba
Asili/Mbadala Dkt. Paul Mhame wakati wa kikao kazi cha usambazaji wa
miongozo inayosimamia huduma za tiba katika ukumbi wa Chimwaga jijini
Dodoma.
Dkt. Mhame amesema kuwa miongozo
hiyo itakayowasilishwa kwa siku mbili imesisitiza kuboresha utoaji wa
huduma za tiba pia masuala ya usimamizi wa huduma za damu salama pamoja
na sheria, kanuni na miongozo ya kusimamia Tiba Asili nchini.
“Hakikisheni masuala haya ambayo
ni mtambuka katika utoaji wa huduma mnayaelewa vyema ili muweze
kuisaidia jamii, ikumbuke kuwa yapo maelekezo yaliyotolewa na viongozi
wa kitaifa hususan suala la tiba asili na tiba mbadala hivyo muhakikishe
mnawawezesha waratibu hao pindi inapotokea changamoto katika kusimamia
huduma hizi kwenye ngazi mnazosimamia”.Alisisitiza Dkt. Mhame.
Hata hivyo Dkt. Mhame aliwataka
washiriki hao kuhakikisha ujumbe utakaotolewa kwenye kikao kazi hiko
kitawafikia walengwa ili pindi ukaguzi na usimamizi shirikishi
utakapofanyika uwe na tija katika kuboresha huduma za tiba kwenye maeneo
waliyotoka na hivyo itasaidia kuboresha huduma za uchunguzi katika
hospitali na ngazi mbalimbali za utoaji huduma za tiba nchini.
Naye Mkuu wa huduma za Maabara
nchini kutoka Wizara ya Afya Peter Torokaa amewasisitiza vituo vyote vya
kutolea huduma za afya nchini kufanyia tathimini ya ufanisi
“Calibration” wa mashine zote kwa kuwatumia wataalam wa maabara na zile
zinazotakiwa kufanywa na Shirika la Viwango (TBS) wanafanyia pia kwani
ndio wenye mamlaka.
Aidha, Torokaa amewataka
Mameneja na Waratibu wa maabara wa Mikoa na Wilaya kuhakiki uwezo wa
mashine “Method Verification” kupima na kutoa majibu yaliyo sahihi hivyo
kila kipimo kithibitishwe kama kinatoa majibu ya wagonjwa yaliyo
sahihi.
“Jambo la tatu tunalosisitiza ni
wataalam wetu kupimwa umahiri kwa kuhakikisha mameneja na waratibu wetu
wa Mikoa na wilaya wanasimamia watoa huduma wetu ambao ni wataalamu wa
maabara wanafanyiwa umahiri kama wana uwezo wa kutumia hiyo
mashine,kifaa na kutoa majibu ikiwemo uwezo wa tafsiri majibu ambayo
yanaenda kwa Daktari kufanya maamuzi kwa mteja.
Aliongeza kuwa kila kipimo
lazima kifanyike kidhibiti ubora kabla maabara haijatoa majibu kwenda
kwa daktari kuhakikisha inadhibiti majibu hayo ndani ya maabara kwa kila
kipimo pamoja na kuhakikisha maabara inashiriki sampuli zingine ndani
na nje ya nchi ili kuweza kujipima kama wanaweza kutoa majibu yaliyo
sawa.
Naye Meneja wa Maabara wa
Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tanga-Bombo Sinde Mtobu amesema maabara
yao imekuwa miongozi wa uboreshaji wa huduma nchini na kuwa katika ngazi
ya nyota nne hivyo wanasubiri kupata ithibati ya kimataifa IS0-15-18-9
kwenye huduma za ubora kwa ujumla hivyo wapo miongoni mwa maabara 27
nchini.
Ametaja moja ya eneo ambalo
wamefanya vizuri kwenye maabara ni kuwawezesha wataalam wa maabara
kwenye umahiri kwa kusimamia miongozo yote pamoja na eneo la uhakiki
ubora wa huduma zao kabla ya kwenda kwa daktari.
No comments:
Post a Comment