Pages

Tuesday, December 1, 2020

MKAZI WA BIHARAMULO AIBUKA MSHINDI WA GARI KWENYE PROMOSHENI YA SHANGWE SHANGWENA NA M PESA ‘WATEJA WATANO WAZAWADIWA SH.MILIONI 1 KILA MOJA


Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano Vodacom Tanzania PLC,  Jacquiline Materu akiongea na mmoja kati ya washindi waliojishindia kitita cha shilingi milioni moja wakati wa kutangaza washindi waliojishindia bahati nasibu ya promosheni ya Vodacom Shangwe Shangwena iliyochezwa leo ambapo watumiaji watano wa  Vodacom M-PESA wamejishindia pesa taslimu shilingi milioni moja na mmoja wao bi Happyness Manembe Appolo kutoka wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera kujishindia Gari aina ya Renault KWID. Jumla ya magari matano, pesa taslimu shilingi milioni 25 na zawadi zenye thamani ya zaidi ya shilingi 3 bilioni kutolewa ndani ya wiki 5. Kuongeza nafasi ya ushindi fanya miamala ya M-Pesa kadri uwezavyo msimu huu wa sikukuu.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko Vodacom Tanzania PLC, Nandi Mwiyombella (katikati )  akichezesha droo ya promosheni ya Vodacom Shangwe Shangwena iliyochezwa leo ambapo  zawadi ya kwanza ya gari aina ya Renault KWID imekwenda kwa Happyness Manembe Appolo mwenye umri wa miaka 46 mkazi wa Biharamulo mkoani Kagera. Jumla ya magari matano, pesa taslimu shilingi milioni 25 na zawadi kemkem zenye thamani ya zaidi ya shilingi 3 bilioni kutolewa ndani ya wiki 5. Kuongeza nafasi ya ushindi fanya miamala ya M-Pesa kadri uwezavyo msimu huu wa sikukuu. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano Vodacom Tanzania PLC, Jacquiline Materu na Mwakilishi toka Bodi ya michezo ya kubahatisha, Rasul Masoud

 

No comments:

Post a Comment