***************************************
NJOMBE
Wahamiaji haramu 16
kutoka Somalia wamekamatwa kwa nyakati tofauti na vikosi vya patro vya
uhamiaji vya kituo kidogo cha Makambako mkoani Njombe wakijaribu kuvuka
nchini ili kufika Africa ya Kusini
Wahamiaji 12 kati ya
16 wamekamatwa wilayani Wanging’ombe wakiwa ndani ya gari aina ya Nissan
Caravan yenye nambari za usajiri T 865-DQA ambapo wameingia nchini
kupitia mpaka wa Namanga wakitokea nchini Kenya huku wengine 4
wakikamatwa ndani ya Reli ya TAZARA mjini Makambako.
Akizungumzia matukio
hayo mkuu wa idara ya uhamiaji mkoani humo kamishna msaidizi mwandamizi
john yindi amesema jeshi limejipanga vyema kudhibiti wahamiaji haramu
kwa kufanya doria masaa 24 na kwamba katika tukio la kukamatwa kwa
wahamiaji 12 dereva na kondakta ambao ni watanzania walifanikiwa
kutoroka na kuacha gari lao.
Kuhusu hatua
zinazochukuliwa kwa wahamiaji hao Kamishna Yindi amesema tayari jitihada
za kuwafikisha mahakamani zimefanyika huku pia akitoa onyo kwa mtu
yeyote anayejihusisha na biashara ya kuingiza wahamiaji haramu nchini
kwani atafikishwa mahakamani pia na chombo chake kutaifishwa.
Takribani Magari
matatu ya watanzania wazalendo yanashikiliwa wakati kesi zikiendelea kwa
kuhusika wanaotuhumiwa kuhusika na biashara hiyo chafu.
No comments:
Post a Comment