Toleo jipya la simu ya Infinix 8 Note iliyozinduliwa hivi karibuni imebeba processor aina ya Helio G80 ikiwa ndio sifa kuu kwa simu hiyo na kupelekea kuvunja rekodi yake yenyewe kwa kuja na simu janja yenye mfumo wa kukidhi mahitaji ya wadau wenye matumizi makubwa ya simu.
Infinix NOTE 8 imekuja na sifa nyengine zenye kuifanya simu hiyo kuwa ya
kipekee kama vile 64MP Ultra HD 6, Battery mAh 5200, kioo cha nchi
6.95, Android 10.
Processor
MediaTek Helio G80 processor ikichagizwa na MediaTek HyperEngine Game
Technology ambayo inaipa nguvu simu hiyo na kuiwezesha kufanya kazi kwa
haraka na kuhakikisha kuwa simu hiyo inagusa maeneo mengine yote ya
kimsingi kwa ufanisi. Chipset yenye sifa ya kufanya kazi vizuri
imefungwa katika simu hiyo si tu kuifanya iwe nyepesi wakati wa matumizi
bali inaifanya kuwa imara zaidi.
Inarahisisha games zinazochukua muda mrefu kufunguka kwa haraka na
kucheza kwa ufanisi, zinatumika katika maeneo maalum na games zenye
ukubwa. Simu hii imeongezewa ufanisi wa hali ya juu na maboresho ya
uunganishwaji kwa minajili ya kuwezesha mtu kucheza game bila bughudha.
Battery
Infinix NOTE 8 imebeba ujazo wa battery yenye mAh 5200M lengo ni kuona
mtumiaji wa Infinix Note 8 anaifurahiya simu yake kwa muda mrefu pasipo
hofu ya kuzima chaji lakini pia hujaa chaji kwa haraka. hii inapewa
nguvu na teknolojia ya hali ya juu (power marathon) iliyomo ndani ya
simu janja ambayo hata kama chaji inakwisha inaiwezesha kutunza chaji
kwa muda fulani. Kwa wapenzi wa games, hii itawahakikishia wanakuwa na
muda mrefu wa kucheza au kutazama na Kwa mfanyabiashara au mjasiriamali
aliyefanikiwa, Note 8 inakupa uhakika wa haya yafuatayo kwa urahisi kama
vile kutuma barua pepe, kutumia apps zinazohusu shughuli za kiofisi,
kutumia apps za kufanya mikutano kupitia video na mengine zaidi.
Vile vile simu hii ina teknolojia ya injini mbili. Jambo hili linaifanya
Infinix Note 8 kuwa ya baridi, ikipunguza joto kwa jotoridi 8 wakati
inachajiwa.
Kamera
Moja ya sifa kubwa zinazoitofautisha simu hii na simu nyingine ni kuwa
na kamera kubwa mbili 64MP Ultra HD 6nyuma na 16MP mbele. Kioo chake
kikiwa na uwiano wa 20.5:9 ambacho kina kamera ndogo mbili ambapo
inakiwezesha kioo cha simu hiyo kuzunguka kufikia eneo la kamera kiasi
cha kutoleta usumbufu ukiitumia kuangalia video kwenye simu.
Simu hiyo yenye kioo chake cha kisasa (6.95" Dual Infinity-O Display)
kinasaidia kamera kuchukua picha zenye ubora kwa kuhakikisha hakuna
vizuizi vyovyote vitakavyoharibu ubora wa picha.
Infinix pia imepata suluhisho la kukabiliana na mazingira ya mwanga
mdogo ambalo limekuwa likiwasumbua watumiaji wakati wakichukua video.
Kwa kutumia zaidi ya siku 180 (usiku na mchana) kufanya utafiti na
maboresho kukabiliana na suala hili, simu hii ina mfumo maalumu wa
kuiwezesha simu kufanya kazi katika mazingira ya giza (Note 8’s Ultra
Night Mode 2.0) inakupa matokeo mazuri katika mazingira yenye mwanga
hafifu.
Muonekano
Muonekano wake utaweza kuwavutia watu mbalimbali na kwa namna simu hii
ilivyo umuhimu wake utaongezeka maradufu kama ambavyo ilivyo muhimu kwa
mtu kuvaa nguo mwilini mwake. Simu hii ina muundo mwepesi sambamba na
GEM CUT ambayo imebuniwa kwa kuangalia mitindo inavyokwenda na hadhi
yake. Uumbaji wa simu hii ambao bado ni mfano wa kuigwa umebebwa na
mistari ya kipekee na uhalisia wa teknolojia. Muundo wake wa Gem Cut ni
mahususi kwa ajili ya kubadili muonekano wa mtumiaji.
Mapokezi
Ukipitapita madukani na kwenye mitandao ya kijamii utagundua ni simu
iliyopokelewa vizuri sana na hii ni huenda na wanachokipromoti ndicho
wateja wanachokutana nacho baada ya ununuzi, Infinix NOTE 8 imepokelewa
vizuri na watu wa rika lote hasa wale wenye kuitumia simu kama chombo
muhimu katika shughuli za kila siku za kujipatia kipato.
Upatikanaji
Infinix NOTE 8 inapatikana kwa bei isiyozidi sh. 540,000 katika maduka yote ya simu nchini Tanzania ikiwa na ofa ya GB 96 kutoka Vodacom lakini pia unaweza tembelea https://www.infinixmobility.com/tz/ .
No comments:
Post a Comment