Pages

Sunday, November 29, 2020

MWENYEKITI BODI YA NISHATI VIJIJINI AWASHA UMEME KITUO CHA AFYA KWAMTORO DODOMA ‘WANANCHI WAMSHUKURU RAIS MAGUFULI’

Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Wakili Julius Kalolo,akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kwamtoro kabla ya kuwasha umeme katika kituo cha Afya cha Kwamtoro kilichopo Chemba Mkoani Dodoma

Mkurugenzi wa Bodi ya Nishati Vijijini, Mhandisi Styden Rwebangira ambye pia ni Naibu Kamishna wa Umeme wa Wizara ya Nishati,akiwaelezea wanakijiji wa Kwamtoro jinsi ya kutumia kifaa cha Umeme (Umeta) akikionyesha kabla ya Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Wakili Julius Kalolo kuwasha umeme katika kituo cha Afya cha Kwamtoro kilichopo Chemba Mkoani Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi za REA, Mhandisi Jones Olotu ,akielezea  Mradi huo ulivyohusisha ujenzi wa kilomita 47 za njia ya msongo wa kati na kilomita 25.2 za njia za msongo mdogo za usambazaji wa umeme pamoja na ufungaji wa vipoza umeme sita. 

Mwenyekiti wa Kijiji cha Kwamtoro Hussein Chande,akitoa maelezo juu ya changamoto ambazo wamekuwa wakizipata (kushoto) ni Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Wakili Julius Kalolo ambaye aliwasha umeme kwenye kituo cha Afya cha Kwamtoro kilichopo Wilayani Chemba Mkoani Dodoma.

Mwanakijiji Bi.Alpha Athuman akielezea furaha walioipata mara baada ya kupata umeme ambao utawasaidia katika kuleta maendeleo katika kijiji chao cha Kwamtoro kilchopo Chemba Mkoani Dodoma ambapo Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Wakili Julius Kalolo aliwasha umeme kwenye kituo cha Afya cha Kwamtoro.

Mwanakijiji wa Kwamtoro Bw.Ayubu Seleli akielezea changamoto zilizopo katika kijiji hicho kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Wakili Julius Kalolo (hayupo pichani) ambaye aliwasha umeme katika kituo cha Afya cha Kwamtoro kilichopo Wilayani Chemba Mkoani Dodoma.

Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Wakili Julius Kalolo (hayupo pichani) wakati akiwahutubia kabla ya kuwasha umeme katika kituo cha Afya cha Kwamtoro kilichopo wilayani Chemba Mkoani Dodoma.

Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Wakili Julius Kalolo,akiwasha umeme  katika kituo cha Afya cha Kwamtoro kilichopo Chemba Mkoani Dodoma

………………………………………………………………………………………

Na.Alex Sonna,Chemba

Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Wakili Julius Kalolo amewasha umeme katika

kituo cha Afya cha Kwamtoro kilichopo Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma ikiwa ni ishara ya kukamilika kwa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili katika Kijiji hicho.

Akizungumza mara baada ya kuwasha umeme huo Wakili Kalolo amewataka wananchi kutunza  miundombinu ya kusambaza umeme na kutoa taarifa ya uharibifu wa miundombinu hiyo kwa uongozi wa Kijiji ili ziweze kutafutiwa ufumbuzi.

”Kumbukeni Miundombinu inajengwa kwa gharama kubwa tunaomba muilinde, kama mtaona nguzo imeanguka au uharibifu toeni taarifa kwa uongozi wa kijiji ili waweze kuwasaidia kwa uharaka”amesema Wakili Kalolo

 Wakili Kalolo amesema kuwa Mradi wa Ujazilizi umezinduliwa mwezi Septemba 2020 kwa ajili ya kusambaza umeme katika vitongoji na maeneo ambayo hayapelekewa umeme.

Naye Mkurugenzi wa Bodi ya Nishati Vijijini, Mhandisi Styden Rwebangira ambye pia ni Naibu Kamishna wa Umeme wa Wizara ya Nishati amesema kuwa atakutana na REA na TANESCO ili kuhakikisha vifaa vya umeme vinafungwa na kuwawezesha wananchi kupata huduma ya umeme bila kero.

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi za REA, Mhandisi Jones Olotu amesema kuwa Mradi huo ulihusisha ujenzi wa kilomita 47 za njia ya msongo wa kati na kilomita 25.2 za njia za msongo mdogo za usambazaji wa umeme pamoja na ufungaji wa vipoza umeme sita. Gharama ya Mradi huo ni bilioni 2.93

Mwenyekiti wa Kijiji cha Kwamtoro Hussein Chande  amesema kuwa pamoja na kuwashiwa umeme kumekuwa na changamoto mbalimbali ambazo alizitaja kuwa ni kuchelewa kupatiwa Namba ya kumbukumbu ya malipo kutoka TANESCO ili waweze kulipia gharama za kuunganishiwa umeme na waliowashiwa umeme mita zao hazijawekewa seal hivyo umeme unapoisha hawawezi kununua.

Kwa upande wa wananchi wa Kwamtoro wameishukuru Serikali kwa kuwaletea umeme ambao utawanufaisha katika kuleta maendeleo kwa ujumla katika kijiji hicho.

”Kwa kweli tumshukuru Rais Magufuli kwa kuteletea umeme kwani kwa muda mrefu lilikuwa changamoto kwenu kwani wakina mama walikuwa wanapata shida wakati wa kujifungua ila kwa sasa itaongeza morali kwa wanafunzi wetu kwa kujisomea wakati wa usiku hii ni faraja kubwa pia kwa wajasiriamali wetu”wamesema wanakijiji

 

No comments:

Post a Comment