Pages

Sunday, November 29, 2020

MAADHIMISHO YA MIAKA 100 YA HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA DODOMA YAFANA

Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa

ya Mkoa wa Dodoma, Dk Ibenzi Ernest akimuongoza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,

Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Profesa Mabula Mchembe (aliyevaa kaunda

suti) na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tamisemi, Dk. Doroth Gwajima  (wa tatu kulia) kwenda kuzindua ukarabati wa chumba cha dharula na

uangalizi wa wagonjwa mahututi  (ICU), 

wakati wa maadfhimisho ya miaka 100 tangu Hospitali hiyo hiyo ianzishwe

1920. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya

Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Profesa Mabula Mchembe  (wa pili kushoto ) akikata utepe kuzindua rasmi ukarabati wa chumba cha dharula na uangalizi wa

wagonjwa mahututi (ICU), katika Hospitali hiyo. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tamisemi, Dk. Doroth Gwajima. 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya

Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Profesa Mabula Mchembe akikagua chumba cha

uangalizi wa wagonjwa mahututi (ICU).

 

Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Dk Ibenzi Ernest akimuongoza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Profesa Mabula Mchembe kukagua wodi ya wanawake ambayo imekarabatiwa na kuwekwa vifaa vipya ikiwemo vitanda, magodoro na vinginevyo.

 

 

Jengo la Wazazi

Jengo la Bima ya Afya

Wanafunzi wa Chuo cha Afya Mirembe, mkoani

Dodoma wakitumbuiza kwa wimbo maalumu wakati wa maadhimisho hayo.

Sehemu ya wafanyakazi na wageni waalikwa

 

 

Naibu

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tamisemi, Dk. Doroth Gwajima  akitoa neno  wakati wa maadhimisho hayo.

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde akitoa ahadi ya kujenga choo na bafu eneo la wananchi wanaosubiria wagonjwa wao katika Hospitali hiyo.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Dodoma Mjini, Meja mstaafu John Salingo akielezea kuwa mafanikio ya Hospitali hiyo ni Utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Baadhi ya watumishi na wageni waalikwa waliohudhuria maadhimisho hayo.

 

 

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Best

Magoma akitoa nasaha zake wakati wa maadhimisho hayo.

Aliyekuwa Muuguzi Mkuu wa Mkoa  Anatolia Mkindo akikabidhiwa cheti cha

kutambua mchango wake katika hospitali hiyo kabla ya kustaafu.  Baadhi ya watumishi wa hospitali waliostaafu

walitunukiwa vyeti.

 

Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali hiyo, Dk.

Ezekiel Mpuya akimkabidhi tuzo  maalumu

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,

Profesa Mabula Mchembe.

Happy Mwaikugile ambaye ni mmoja wa wafanyakazi bora akilakiwa kwa furaha na wafanyakazi wenzie baada ya kutunukiwa tuzo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya

Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Profesa Mabula Mchembe (kulia) akimkabidhi tuzo

maalumu Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Dk Ibenzi

Ernest kwa uongozi wake thabiti.

 

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Best

Magoma akitoa nasaha zake wakati wa maadhimisho hayo.

 

No comments:

Post a Comment