Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan
Abbasi akitoa maagizo kwa Watendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania kuratibu
ushiriki wa Wasanii wa Filamu na BASATA kuratibu ushiriki wa Wasanii wa
Muziki katika kazi za serikali kwa lengo la kuepuka mawakala wanaoleta
migogoro miongoni mwao, leo Novemba 30,2020 jijini Dar es Salaam
katika kikao na wakuu wa taasisi zinazosimamia sekta ya sanaa nchini .
Mtendaji Mkuu Taasisi ya
Hakimiliki na Hakishiriki (COSOTA) Doreen Sinare akimshukuru Katibu Mkuu
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa
Serikali Dkt. Hassan Abbasi (hayupo pichani ) kwa kuwasaidia kupata mdau
wa usambazaji kutoka india atakayeshirikiana wasambazaji wa filamu
nchini wanaofanya tafsiri ya filamu za kihindi, leo Novemba 30, 2020
Jijini Dar es Salaam katika kikao na wakuu wa taasisi zinazosimamia
sekta ya sanaa nchini .Katibu
Mtendaji Baraza la Sanaa Tanzania Godfrey Mngereza akimshukuru
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji
Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi kwa maelekezo aliyoyatoa kwa baraza
kuratibu ushiriki wa wasanii wa muziki katika shughuli za serikali ,
leo Novemba 30, 2020 Jijini Dar es Salaam katika kikao na wakuu wa
taasisi zinazosimamia sekta ya sanaa nchini .
****************************************
Na Anitha Jonas – WHUSM, Dar es Salaam
30/11/2020
Katibu Mkuu Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.
Hassan Abbasi amewataka Wakuu wa Taasisi zinazosimamia Sekta ya Sanaa
nchi kuandaa mikakati itakayosaidia kukuza na kuendeleza sekta hiyo.
Dkt. Abbasi ametoa
kauli hiyo Leo Novemba 30, 2020 Jijini Dar es Salaam katika kikao na
viongozi chenye lengo la kutafuta suluhu ya namna bora ya kuendeleza
sekta ya Sanaa nchini.
Katika kikao hicho
Katibu Mkuu huyo alisisitiza kuwa Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli katika hotuba yake mara baada ya
kuapishwa na katika ufunguzi wa Bunge pamoja na katika Ilani ameeleza
lengo la kuendeleza Sekta ya Sanaa.
Akizungumza katika
kikao hicho kilichokuwa na Wakuu kutoka BASATA, COSOTA, Bodi ya Filamu
na TaSuBa alisisitiza kuwa lazma Sekta ya Sanaa ijipange kuwa na
miundombinu mbinu yake ya kisasa itakayoendeleza kazi hiyo ikiwemo
ujenzi wa “sport arena”.
“Sasa ni wakati wa
kuangalia namna ya kutatua changamoto za kisekta na siyo changamoto
binafsi tuangalie mambo gani yaboreshwe kama ni Sera, Sheria au
Kanuni”alisema Dkt.Abbasi.
Pamoja na hayo Dkt.
Abbasi alitoa maagizo mbalimbali kwa Wakuu hao ikiwemo kuandaa mpango
wa kutoka mafunzo mbalimbali, na kwa TaSUBa kujipanga kuwa na kozi za
muda mfupi utoaji zitakazosaidia wasanii.
Vilevile Katibu Mkuu
huyo alitoa maagizo kwa Bodi ya Filamu kusimamia na kuratibu shughuli
zote za Serikali zitakazohitaji na Wasanii Wafilamu na kwa upande wa
Muziki BASATA nao ndiyo kuwa waratibu hii ni kwa lengo la kuondoa
mawakala miongoni mwao ambao huchangia kuleta changamoto mbalimbali.
Aidha, Dkt. Abbasi
pia ameitakaTaasisi ya COSOTA kutafuta mfumo bora wa kieletroniki
utakaosaidia ukusanyaji wa mapato ya kazi za wasanii pamoja na namna
bora ya kutumia mifumo ya kidijitali katika kulinda haki za wasanii ili
waweze kufaidika na kazi zao.
Kwa upande wa
Mtendaji Mkuu COSOTA Doreen Sinare alimshukuru Katibu Mkuu huyo kwa
kupata wadau kutoka India, ambao watashirikiana na wasambazi wa kazi za
Filamu Tanzania ambao wanafanya tafsiri ya filamu za kihindi ili kupata
ridhaa ya Wamiliki wa Filamu za india zifanyiwe tafsiri
No comments:
Post a Comment