Mkuu wa Wilaya ya Ilala – Ng’wilabuzu Ludigija, akimkabidhi cheti cha shukrani kwa Benki ya NMB, Meneja Mwandamizi Idara ya Biashara za Serikali wa NMB – Adelard Mang’ombo, kama mmoja wa wadau walipa kodi wakati wa Siku ya Mlipa Kodi katika Manispaa ya Ilala.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala – Ng’wilabuzu Ludigija, akizungumza na Meneja Mwandamizi Idara ya Biashara za Serikali wa NMB – Adelard Mang’ombo baada ya kukabidhiwa cheti cha shukrani kwa Benki ya NMB kwa mmoja wa wadau walipa kodi wakati wa Siku ya Mlipa Kodi katika Manispaa ya Ilala. Kushoto ni Meneja Mwandamizi Uhusiano Biashara na Serikali wa NMB – Amanda Feruzi na Meneja Mauzo ya Kidijitali – Hezbon Mpate.
………………………………………………………………………………..
Benki ya NMB imetajwa kuwa taasisi kinara ya kifedha katika Manispaa ya Ilala mkoani Dae es salaam inayotumia kiasi kikubwa cha pato lake kuisaidia jamii katika Nyanja za Elimu na Afya
kupitia Mpango wake wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR).
Kupitia mpango huo Benki hiyo imekuwa mstari wa mbele kati ya taasisi nyingi za fedha kwenye mkoa huo, ambayo imekuwa ikishirikiana na serikali kuhakikisha huduma bora za kiafya na elimu zinapatika kwa wananchi.
Hatua hiyo ilipelekea Manispaa hiyo kuipatia Benki hiyo cheti cha Pongezi, kwenye hafla ya kufunga wa kongamano la siku ya mlipakodi lilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.
Katika hafla hiyo, Manispaa ya Ilala ilikabidhi vyeti kwa taasisi, mashirika, makampuni na wafanyabiashara 100 Bora wa Ulipaji Kodi Bila Shuruti, huku NMB ikipongezwa na kutunukiwa kama Kinara wa matumizi ya pato lake katika kusaidia jamii.
Akiongea katika kongamano hilo, Meneja Uwajibikaji Miradi ya Jamii – Lilian Kisamba, alisema kuwa toka mwaka 2020 hadi leo Benki hiyo imetoa shilingi Milioni 218.9 katika mkoa wa Dar es salaam kwenye miradi inayogusa jamii moja kwa moja.
Alisema kuwa kati ya fedha hizo kiasi cha Shilingi Milioni 153.9 zimetumika katika sekta ya Elimu na Millioni 65 ikienda kwenye Afya, ambapo jumla ya shule 26 zimepokea madawati 300 na kusaidia watoto 3900 ambao walikuwa wanakaa chini kwa kukosa madawati.
Aliongeza kuwa shule sita zilipatikwa msaada wa mabati yenye thamni ya shilingi Milioni 40, ambapo mkuu wa Wilaya hiyo Ng’wilubuzu Ludigija wakati akikabidhi cheti hicho cha pongeza aliishiruku benki hiyo kwa juhudi zake.
No comments:
Post a Comment