Vijana katika halmashauri ya Wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera wameaswa kutosubiri ajira kutoka serikalini bali wajikite katika kujiajili haswa katika kilimo,uvuvi na ufugaji ili kuweza kujikwamua na umasikini.
Hayo yamesemwa na bwana Agape Ishabakaki wakati akizungumza na mpekuzi blog ambaye pia ni mratibu wa shirika lisilo la kiserikali la FUAP TANZANIA linalojiusisha na masuala ya kusaidia wakulima na wafugaji ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ya watu haswa vijana ili kujenga utamaduni wa kujiajili uku wakiwa wamesubiri ajira kutoka serikalini.
Bwana Agape amesema kuwa shirika hilo kwa sasa limetua mkoani Kagera hususani katika wilaya ya Missenyi na litazungukia kata mbalimbali ili kutoa elimu kwa vijana juu ya faida za kujiajili na kutoa elimu kwa vijana hao kujikita katika kilimo kwa manufaa yao ya badae .
Katika hatua nyingne bwana Agape amesema kuwa zaidi ya miti elfu kumi ya matunda itazalishwa na shirika hilo na zoezi hilo litaanza tarehe mbili mwezi wa kumi katika kata ya Bugorola ili kuwapa fursa vijana pamoja na wananchi wa Missenyi kuwa na elimu juu ya utunzaji mazingira pamoja na kuwa na utamaduni wa kupanada miti katika maeneo yaliyowazunguka.
Kwa upande wake mkurugenzi wa shirika hilo bwana Josephat Joseph John amesema kuwa kwa sasa hivi shirika ilo lina mradi unaoitwa AGRI EXPERIENCE ambapo mradi huo utawawezesha vijana wengi kujifunza na kujua namna ya kufuga kuku wa kisasa pamoja na kufahamu ujuzi mbalimbali wa biashara ya mayai ya kisasa, ufugaji wa nyuki nk.Bwana Josephat amesema kuwa vijana watumie shirika hilo vizuri kwa kuwa elimu itatolewa bila malipo yoyote na ku ongeza kuwa kabla yakuondoka mkoani hapa vijana wawe wameisha pata maarifa na ujuzi wa kujiajili wenyewe kupitia kilimo na ufugaji wa kisasa uku akitaja kauli mbiu yao kuwa ni “Kijana wa kagera kulima kwa tija kwa maendeleo yao wenyewe na taifa kwa ujumla 2020-2025”.
No comments:
Post a Comment