Mwanamke Mtanzania mfanyabiashara aishiye Marekani(UK) ,Gladness Katega akiongea na waandishi wa habari juu ya kongamano la wanawake wafanyabiashara aliloliandaa.
………………………………………………………..
Na Woinde Shizza,Arusha
Mwanamke Mtanzania
mfanyabiashara aishiye Marekani(UK) ,Gladness Katega Amewataka wanawake
kujitokeza katika kongamano la wajasiliamali linalotarajiwa kufanyika
mnamo Oktoba 2 na 3 ili kujifunza na kujadili changamoto za kibiashara
ili kuweza kupanua biashara zao na kumuinua mwanamke kiuchumi.
Aidha pia Alisema
kuwa mbali na wanawake pia litakuwa na kongamano lingine ambalo
litafanyika October 5 na 6 ambalo litawakutanisha wanaume na kujadili
changamoto mbalimbali wanazokutana nazo
Akizungumza na
waandishi wa habari jijini Arusha,Katega alisema kongamano hilo
litawasaidia wanawake wa Tanzania katika kuinuka kiuchumi na kuweza
kutanua biashara zao
Alibainisha kuwa
lengo lao kubwa la kufanya kongamano hili ni kuwaweka wanawake pamoja
na kuona wanafanya biashara kwa pamoja na kuinuka
Alisema kuwa
kongamano hilo litashirikisha wanawake hapa nchini pamoja na nchi
mbalimbali ikiwemo Marekani ,Uingereza,Ghana ,Zimbabwe , Southafrika
pamoja na Kenya na hasi Sasa zaidi ya wanawake 100 wameshathibitisha
kishiriki
Alisema kuwa wanataka
kuona mwanamke anainuka kiuchumi anatoka hatua moja anaenda hatua
nyingine na anafanikiwa na pia napenda kuona wanawake wakibebana
wakisaidiana ili waweze kufika mbali na kongamano hili litawasaidia
kupata elimu watapata mafunzo watajadiliana namna ya kukuza biashara
nakufikia Mataifa mengine
Alisema mgeni rasmi
wa kongamano hili anatarajiwa kuwa ni Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Anna
Mghwira huku akitaja wathamini wa kongamano hili kuwa ni Burka Coffee
Logle ,Duluti garden,Mrembo safari,TTB,sunbright hotel,partner Africa
Investment,na Kipina beauty saloon .
Alitoa wito kwa Kila
mwanamke na mwanaume kuhuthuria ili kuweza kupata mitandao ya
kibiashara nakujua namna ya upatikanaji wa masoko pamoja na kutatua
changamoto ya namna ya kukuza biashara zao ,pamoja nanamna ya kufanya
biashara kimataifa ukizingatia katika kipindi hichi ambacho baadhi ya
nchi bado zinakabiliwa na janga la ugonjwa wa covid 19
Naye mwezeshaji wa
mfunzo ya wanaume ya Kings master class kutoka nchini Kenya ambaye ni
mkurugenzi wa kampuni ya RB, Dk.Robert Burale alisema wanaume wengi
wanatunza maumivu moyoni na kushindwa kuyasemea kwa watu kuhusu hali ya
maisha pamoja na changamoto ambazo wanakutana nazo Ndani ya familia
kitu ambacho hufanya baadhi ya wanaume kupoteza maisha na wengine
kufanya maamuzi ambayo Sio mazuri
“mwanamke anaweza akapata kitu akachukuwa sumu akanywa ,au hata akajinyonga lakini kwa mwanamme anaweza akaumizwa na kitu badala ya kufikiria kijinyonga yeye akachukuwa uamuzi wa moja kwa moja hivyo nitawaeleza namna ya kukabiliana na changamoto hiyo “alibainisha
Aliwataka wanaume
kujitokeza kwa wingi katika kongamano hili ,huku aliwasisitiza wanawake
kuwashauri wanaume wao kwenda katika kongamano ,kwani iwapo watajitokeza
hawata jutia .
No comments:
Post a Comment