Katibu
Mkuu Wizara ya viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe akitoa neno la
ufunguzi wa mdahalo huo kwenye ukumbi wa freedom Square Mazimbu
Morogoro.
Washiriki wa mkutano huo kutoka Vyuo vikuu, Taasisi za Utafiti na
Mashirika ya Kise rika ku na yasiyo ya Kiserikali kutoka mikoa
mbalimbali nchini.
Mkuu
wa Mradi wa CREPEE Dkt. Faith Mabiki akizungumza kuhusu malengo ya
Mradi na mdahalo huo wakati wa Ufunguzi wa mdahalo huo.
Naibu
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Maulid
Mwatawala akizungumza kwa niaba ya Makamu mkuu wa chuo Prof. Raphael
Chibunda wakati wa ufunguzi wa Mdahalo huo.
Picha ya pamoja ya Katibu Mkuu Prof. Shemdoe na Viongozi wa SUA na Mradi wa CREPEE Mara baada ya ufunguzi wa Mdahalo huo.
*************************************
Serikali inategemea matokeo ya
Tafiti katika kufanya maamuzi na kusimamia maendeleo ya nchi ingawa
mchango wa tafiti hizo katika kutunga sera na mipango ya maendeleo
nchini sivyo ya
kuridhisha.
Hayo ya yamesemwa na Katibu Mkuu
Wizara ya viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe wakati akifungua
Mdahalo wa wazi wa uchambuzi wa matokeo ya Tafiti katika utunzi wa sera
na mipango ya maendeleo uliyofanya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA
Mkoani Morogoro.
Prof. Shemdoe amesema matokeo
mengi ya Tafiti na taarifa za kitaalamu zinaishia kwenye majarida na
makabati ya maktaba na ofisi wakati ukuaji wa uchumi unategemea
Tafiti,Ubunifu na Uvumbuzi hivyo ni wazi kuwa serikali, vyuo
vikuu/Watafiti na Wazalishaji ni vitu vitatu vinavyotegemeana.
“Serikali yetu imeazimia na kujitolea kuwezesha Taasisi
mbalimbali na Mtafiti mmoja mmoja, kutafiti, kubuni,na kuboresha
teknolojia katika sekta zote za Kiuchumi ikiwemo sekta ya viwanda ambayo
kwa sasa inakuwa kwa kasi kubwa” Alibainisha Prof. Mdoe.
Katibu Mkuu huyo ametoa rai kwa watafiti wote nchini
kuendelea kufanya Tafiti ambazo zitaibua ubunifu katika maendeleo ya
sekta mbalimbali na hivyo mchango wao kupitia matokeo ya Tafiti
kuchangia katika mipango ya maendeleo ya nchi.
Prof. Mdoe amewapongeza SUA kwa wazo hilo zuri kwa
maendeleo ya nchi na kushukuru AIDEP na SUA kwa kifadhili mdahalo huu
wenye lengo la kuanzisha Kituo cha Usanisi wa ushahidi wa Utafiti katika
uundaji wa sera na mipango ya maendeleo nchini.
Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Naibu
Makamu Mkuu wa Chuo Upande wa Taaluma Prof. Maulid Mwatawala kwa niaba
ya Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Raphael Chibunda amesema Sera na Mipango ya
kimaendeleo imekuwa inapungukiwa Urari katika Maendeleo ya Uchumi jamii
na maendeleo endelevu.
Prof. Mwatawala amefafanua kuwa hiyo inatokana na ukweli
kwamba wakati mwingine Tafiti na matokeo ya Tafiti zao hayatumiki
ipasavyo kuakisi mahitaji halisi ya jamii na Taifa katika ujumla wake
lakini pia wanaotunga sera na mipango ya maendeleo hawapati kirahisi na
kwa lugha rafiki matokeo ya Tafiti ili kuyatumia katika utunzi wa sera.
Ameendelea kwa kusema kuwa ni wazi kuwa vyuo vikuu kote
duniani ni joto I cha Taaluma na Tafiti na kwa muktadha huo SUA imeona
ni vyema kutumia uwezo wake wa ndani na kwa kushirikiana na wadau
wengine kuanzisha Kituo cha Usanisi wa matokeo ya Tafiti hapo SUA.
Malengo ya Kituo hicho amesema ni kisanisi ushahidi wa
Utafiti katika uundaji wa sera na mipango ya maendeleo,kufanya mapitio
ya machapisho ya Kisayansi na kuandaa kanzidata ya matokeo mbalimbali ya
Tafiti,kuandaa mihutasari ya matokeo ya Utafiti katika lugha rahisi na
kuandaa mihutasari ya sera.
“ SUA imekuwa na mchango Mkubwa sana kupitia Tafiti za
kisayansi nchini na ulimwenguni kwa mfano kwa matokeo ya yaliyotolewa na
Shirika la webomatrics Mwezi julai 2020, SUA umeshiba nafasi ya
kwanza Kitaifa katika matumizi ya Tafiti zake (citation index) ambapo
zaidi ya watafiti 82,220 duniani watumitumia machapisho ya SUA katika
maandiko yao” Alisema Prof. Mwatawala
Aliongeza “ Mchango huu ni Karibia mara mbili zaidi ya Chuo
kilichoshika nafasi ya pili na ya tatu na ya nne kwa pamoja Kitaifa na
nafasi SUA duniani imepanda kufikia nafasi ya 1161 kati ya vyuo vikuu
Bora 5800 duniani”.
Prof. Mwatawala amesema pamoja na mafanikio hayo Kama Taifa
bado tuma changamoto ambazo zinahitaji kufanyiwa kazi ili kuchochea
matumizi ya Tafiti, Sayansi,teknolojia na ubunifu Kama nyenzo ya
maendeleo ya kiuchumi.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma Prof. Mwatawala amesema
ili kutatua changamoto hizo ni lazima Tafiti zifike ghala na kanzidata
ya ofisi ya takwimu ya Taifa,zitumike katika utunzi wa Sera na mipango
ya maendeleo ya Taifa,ziwafikie wadau wa maamuzi katika lugha rahisi na
inayoeleweka na Pia ziwe na sehemu maalumu kuzichakata na kuzitafsiri na
kuja na hoja mahususi katika Nyanja husika kwaajili ya mipango ya
maendeleo.
Kwa upande wake Mkuu wa mradi wa kujenga na kukuza uwezo wa
Watafiti na watunga sera kuweza kusanisi matokeo ya Tafiti ili
kuchangia kuleta maendeleo nchini CREPEERT Dkt. Faith Mabiki amesema
Afrika ni bara lililo nyuma katika utoaji wa matokeo ya Tafiti licha ya
kuwa na idadi kubwa ya watu.
Ametolea mfano taarifa ya Shirika la elimu, Sayansi na
utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO ya Mwaka 2015 inaonesha bara la
Afrika Linazalisha 2.6% tu ya matokeo ya Tafiti zote duniani lakini pia
Afrika inachangia 2.9% ya watafiti wote duniani.
Dkt. Mabiki amesema kwa takwimu hizo ni kwamba uchangiaji
wa Tafiti kwa maendeleo ya bara la Afrika na Tanzania ni mdogo na hivyo
mradi wa CREPEE Ulizaliwa ili kuchangia katika Juhudi za Serikali
kuongeza uwezo wa watafiti kusanisi matokeo ya Tafiti ili ziweze
kutumika katika maamuzi mbalimbali ya kisera kwa maendeleo ya nchi.
Mkuu huyo wa mradi amesema ili kufikia lengo hilo Mradi
unaendesha warsha za kujenga uwezo na uelewa wa namna Tafiti zinavyoweza
kutumika katika kutoa mamauzi sahihi ya kisera pamoja na midahalo.
No comments:
Post a Comment