Makamu
Rais wa GGML, Simon Shayo (kulia) akimkabidhi kadi ya gari Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Geita, Ali Kidakwa (kushoto.)
Makamu
Rais wa GGML, Simon Shayo (kulia) akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi
wa Kituo cha Afya Bukoli- Geita katika hafla ya kukabidhi gari la
kubeba wagonjwa.
NA MWANDISHI WETU, GEITA.
Kampuni
ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kwa kushirikiana na Rafiki Surgical
Mission kutoka Australia wametoa msaada wa gari la wagonjwa lenye
gharama ya Sh milioni 32 kuhudumia wagonjwa katika kituo cha Afya cha
Bukoli na maeneo jirani wilayani Geita.
Akizungumza
katika hafla ya makabidhiano ya gari hilo katika Kituo cha Bukoli
Wilayani Geita, Makamu Rais anayeshughulikia Mahusiano na Maendeleo
endelevu, Simon Shayo amesema msaada wa gari hilo umetolewa kwa wakati
na utasaidia kutatua changamoto za usafiri kwa wagonjwa mahututi katika
kata hiyo ya Bukoli na maeneo ya jirani.
“Halmashauri
ya Wilaya ya Geita iliomba msaada wa gari la wagonjwa kutoka GGML ili
kuwasaidia wagonjwa katika jamii ya watu wa Bukoli ambao waliokuwa na
changamoto kubwa kila ilipobidi kusafirisha wagonjwa kwa ajili matibabu
makubwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Geita ambayo ipo wastani wa
kilomita 35 kutoka kijiji cha Bukoli.
"
Ushirikiano kati yetu na Rafiki Surgical Mission ni mwitiko wa maombi
hayo na umekuja muda mwafaka kwa kuwa wamekuwa pia na dhamira ya
kusaidia huduma za afya mkoani Geita kwa miaka kadhaa sasa,” alisema Bw
Shayo.
!Kwa
karibu miaka 20 sasa, mbali na kutoa msaada wa vifaa tiba, Geita Gold
Mining Limited kwa kushirikiana na Rafiki Surgical Mission wameongeza
wigo wa matibabu kwa watoto na watu wazima mkoani Geita ambao wamekuwa
wakikabiliwa na changamoto ya midomo sungura na migongo wazi kwa
kuwapatia matibabu ya upasuaji bure.
Bw
Shayo amefafanua kuwa GGML pia walitoa msaada katika kituo cha afya cha
Bukoli mwaka 2004 kwa kujenga jengo la Wagonjwa wa Nje (Outpatient
Department) na nyumba ya watoa huduma wa afya. GGML pia imefadhili
miradi mbalimbali ya afya wilayani Geita ikiwemo ukarabati wa Hospitali
ya Rufaa mkoani Geita na ujenzi wa vituo vipya vya afya katika vijiji
vya Nyamalembo, Nyakahongola, Kasota na Kakubiro ambapo miradi yote hiyo
kwa pamoja iligharimu Shilingi bilioni moja na milioni mia nane (1.8bn)
za Kitanzania.
Mkurugenzi
mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Ali Kidwaka kwa niaba ya
Serikali ametambua mchango wa GGML katika kutatua changamoto ya huduma
za afya katika halmashauri ya wilaya na kwengineko mkoani Geita na
kuwaomba washirika wengine waliopo katika Wilaya ya Geita kushirikiana
na Serikali kwa lengo hilo hilo.
Aidha
mwaka 2019, GGML ilichangia pia vifaa tiba vyenye gharama ya Shilingi
za kitanzania milioni 142 katika vituo vya afya vya Katoro na Bukoli.
No comments:
Post a Comment