Mkuu wa Wilaya ya Geita Fadhil Juma akimkabidhi kitambulisho Cha Toto Afya Kadi kwa mmoja wa Watoto waliojiunga na bima ya afya kwenye hafla ya makabidhiano yaliyofanyika kwenye Banda la Mfuko wa bima ya afya(NHIF).
Mkuu wa wilaya ya Geita Fadhil Juma akiwa katika picha ya pamoja na Watoto na wazazi waliojiunga na Toto Afya Kadi baada ya kuwakabidhi kadi zao.
Meneja
wa Mfuko wa bima ya afya Mkoa wa Geita Elius Odhiambo akimkabidhi mkuu
wa Wilaya ya Geita Fadhil Juma Tshert ya NHIF baada ya kukabidhi kadi za
toto afya kwa watoto kwenye banda la NHIF.
Na Editha Karlo,Geita
MKUU
wa Mkoa wa Geita Enjinia Robert Gabriel ameupongeza mfuko wa bima ya
afya(NHIF)kwakuweka utaratibu mzuri wa kutaka kila mwananchi awe na kadi
ya bima ya afya.
Mkuu
wa Wilaya ya Geita Fadhil Juma ameyasema hayo leo kwenye banda la mfuko
wa bima ya afya(NHIF) akimwakilisha Mkuu wa Mkoa huo kukabidhi kadi za
bima ya afya kwa watoto wenye umri chini ya miaka 18 mpango unaoitwa
toto afya.
Hafla
hiyo ya makabidhiano ya kadi hizo kwa watoto imefanyika kwenye banda la
NHIF kwenye viwanja vya Maonesho ya tatu ya Kimataifa ya Teknolojia na
Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayoendelea Mjini Geita Mkuu huyo wa
Mkoa amewahimiza Watanzania kuchangamkia fursa ya kuwa na bima ya afya
kwa kuwa milango imefunguliwa kwa kila Mwananchi.
"Nina
waomba wananchi kuchangamkia hii fursa ya kila mmoja kuwa na bima ya
afya kwakuwa sasa tayari milango ipo wazi kama mnavyoona serikali yetu
imeboresha sana katika sekta ya afya"alisema
Meneja
wa NHIF Mkoani Geita Elius Odhiambo amesema NHIF inampango wa bima ya
afya kwa kila mtu huku akiyataja hayo makundi yanayosajiliwa kuwa ni
Watumishi,Watoto wenye umri chini ya miaka 18, wanafunzi, wakulima,
wamachinga na watu binafsi.
Makundi
mengine ni wachimbaji wadogo wa madini, madereva, Waendesha boda boda
na wajasiriamali katika vikundi mbalimbali vya kiuchumi.
Odhiambo
alisema viwango vya kujiunga vinatofautina kutokana na kundi ila kadi
za toto afya kadi za watoto wenye umri chini ya miaka kumi na nane ni
shilingi 50,400 kwa mtoto kwa mwaka.
"Siku
zote ugonjwa huwa unakuja bila ya taarifa,kuna siku unaweza kuugua huna
pesa ya matibabu lakini kama una kadi yako wa bima ya afya utakuwa na
uhakika wa matibabu wewe na familia yako hata kama umeugua huna
pesa"alisema Odhiambo.
No comments:
Post a Comment