Pages

Tuesday, September 29, 2020

Benki ya NMB yashiriki mkutano wa vijana wa Umoja wa Mataifa Arusha

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini, Aikansia Muro (kulia) akitoa maelezo kwa mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Mwinyi Haji kuhusu programu za Benki hiyo za kuinua vijana nchini wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa vijana wa Umoja wa Mataifa uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela, jijini Arusha leo.

Wafanyakazi wa Benki ya NMB wakimsikiliza kwa makini Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Mwinyi Haji alipokua akitoa salamu za pongezi kwa Benki hiyo kwa jitihada zao za kuinua vijana nchini.

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini, Aikansia Muro (kulia) akipokea Mkono wa pongezi kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Mwinyi Haji baada ya kuitimisha hotuba yake kuelezea fursa mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo kwa vijana. Anaeshuhudia ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela, Prof. Emmanuel Luoga.

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini, Aikansia Muro akizungumza wakati wa mkutano huo.

**********************************

Benki ya NMB imeeleza kuwa vijana ndio dira ya maendeleo ya sasa na baadaye kwa taifa lolote duniani na ni kundi muhimu la kuzalisha viongozi bora.

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini, Aikansia Muro amesema hayo leo katika

ufunguzi wa mkutano wa vijana walio katika mtandao wa jumuiya za Umoja wa Mataifa nchini (YUNA) unaofanyika katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela jijini Arusha.

Amesema NMB ni benki inayothamini zaidi vijana na imejikita katika kutambua nafasi zao katika ujenzi wa taifa na ukuaji wa sekta ya fedha nchini.

Aikansia amesema benki hiyo inaendesha programu maalumu kwa vijana wanaotoka vyuoni –Graduate Trainee – kujifunza na baadae kupata kazi za kudumu, na kati ya mwaka 2019 na 2020 zaidi ya vijana 50 wameshanufaika na programu hiyo.

“Tukiwa tunatambua umuhimu wa mafunzo kwa vijana kabla ya ajira, kila mwaka tunapokea vijana wenye sifa kuja kufanya mafunzo kwa vitendo huku tukiwapa mikataba ya miezi mitatu mpaka 12. Pia tunapokea vijana kwaajili ya mafunzo wakiwa vyuoni yaani field attachment – na zaidi ya wanafunzi 300 wananufaika na mafunzo haya kila mwaka,” amesema Aikansia.

Mkutano huo ulifunguliwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mwinyi Talib Hajj ambaye alitaka vijana kutumia nafasi wanazopata kujiendeleza kielimu ili kuwa na ushindani katika soko la ajira na fursa za ujasiriamali.

 

No comments:

Post a Comment