Kushoto ni Askofu wa Jimbo Katoliki la
Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu,kulia ni muonekano wa sehemu ya
kanisa iliyoathirika kwa kuangukiwa na mnara wa Redio Faraja
Na Simeo Makoba - Shinyanga
Askofu wa Jimbo Katoliki la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu amewaomba
wadau,waamini na watu wote wenye mapenzi mema kuguswa na kutoa michango
mbalimbali ili kusaidia ukarabati wa miundombinu ya kanisa kuu la jimbo
na Redio Faraja ambayo imeathiriwa na mvua kubwa iliyoambatana na upepo
mkali.
Askofu Sangu ametoa ombi hilo katika kikao cha dharura ambacho
kiliwahusisha Mapadre wa Parokia zote zilizopo katika manispaa ya
Shinyanga,Viongozi wa Halmashauri ya walei kutoka kanisa kuu la Ngokolo
pamoja na uongozi wa Redio Faraja Fm Stereo.
Askofu Sangu amebainisha kuwa,mvua kubwa iliyonyesha mjini Shinyanga
jioni ya jana tarehe 28.09.2020 ambayo iliambatana na upepo mkali
ilisababisha mnara unaotumika kurushia matangazo ya Redio Faraja Fm
Stereo kuangukia kanisa na kusababisha uharibifu mkubwa wa sehemu ya
kanisa na miundombinu ya Redio inayotumika kurushia matangazo.
Shinyanga limeguswa ikizingatiwa kuwa,kanisa kuu la Mama mwenye Huruma
la Ngokolo ndiyo lililobeba sura ya jimbo halikadhalika Redio Faraja
ndiyo chombo kikuu cha mawasialiano na uinjilishaji katika jimbo ambayo
nayo miundombinu yake imeathiriwa.
Askofu Sangu amewaomba wadau wa Redio na Kanisa,Waamini na watu wote
wenye mapenzi mema kuguswa na kutoa michango mbalimbali ili hatua za
kufanya ukarabati wa kanisa na mitambo ya Redio iliyoathiriwa ziweze
kuanza mara moja.
Ameelekeza michango yote iwekwe kwenye Akaunti maalum ya jimbo la Shinyanga Benki ya CRDB yenye namba 01J1058390001 (DIOCESE OF SHINYANGA) na kwa njia ya M-PESA kwa namba 0762444746 yenye jina la Liberatus Sangu.
Wakati huo huo, Askofu Sangu ameunda kamati maalum ambayo itashughulika
na mchakato wote wa tathmini pamoja na kusimamia hatua zote za ukarabati
wa kanisa na miundombinu ya Redio iliyoharibiwa,ambayo itaongozwa na
Paroko wa Parokia ya Ngokolo Padre Aldof Makandagu.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Idara ya mawasiliano
wa jimbo la Shinyanga Padre Anatoly Salawa amesema hivi sasa wanaendelea
na mchakato wa kurejesha matangazo ya Redio katika eneo la Shinyanga
kwa kufunga Antena katika sehemu ya mnara iliyobakia ili kuwawezesha
wananchi wa Shinyanga kufuatilia Matangazo ya Redio wakati hatua
nyingine za kufanyia matengenezo miundombinu iliyoharibiwa zikiendelea.
Mhashamu Baba Askofu Liberatus Sangu akiwa katika eneo la tukio wakati
wa zoezi la kuondoa mnara juu ya paa la kanisa la Mama Mwenye Huruma
Ngokolo. Picha na Samir Salum
Mhashamu Baba Askofu Liberatus Sangu akiwa katika eneo la tukio wakati
wa zoezi la kuondoa mnara juu ya paa la kanisa la Mama Mwenye Huruma
Ngokolo.
Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Jimbo la Shinyanga, Padre Anatoly
Salawa akionesha Mnara wa Matangazo ya Redio Faraja ulioangukia Kanisa
la Mama Mwenye Huruma Ngokolo.
Muonekano wa mnara wa kurushia matangazo Redio Faraja Fm Stereo ukiwa
umeangukia paa la Kanisa Katoliki la Mama Mwenye Huruma Parokia ya
Ngokolo Mjini Shinyanga
Muonekano wa mnara wa kurushia matangazo Redio Faraja Fm Stereo ukiwa
umeangukia paa la Kanisa Katoliki la Mama Mwenye Huruma Parokia ya
Ngokolo Mjini Shinyanga
Muonekano wa sehemu ya ndani ya Kanisa Katoliki la Mama Mwenye Huruma
Parokia ya Ngokolo Mjini Shinyanga baada ya kuangukiwa na Mnara wa
Matangazo ya Radio Faraja Fm Stereo

Ngokolo Mjini Shinyanga.
No comments:
Post a Comment