WAZIRI wa Nchi, OfisiyaRais,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo
akifanya mazoezi ya kukimbia na watumishi wa TAMISEMI kabla ya
kuwasilsha mrejesho kwa watanzania mafanikio ya miaka mitano ya
maboresho ya huduma za afya Msingi chini ya Ofisi hiyo kwenye ‘Siku ya
Afya Tamisemi(AFYA DAY)’ iliyofanyika Jijini Dodoma
WAZIRI wa Nchi, OfisiyaRais,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo
akivishwa medali na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Maswala ya Afya
TAMISEMI , Dkt. Dorothy Gwajima kama ishara ya kumpngeza kwa mafanikio
ya miaka miaka mitano katika sekta ya Afya TAMISEMI leo katika viwanja
vya Michezo Shule ya Sekondari Dodoma
WAZIRI wa Nchi, OfisiyaRais,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo
wakati akitoa zawadi kwa mama aliyejifungua leo katika kituo cha afya
cha Makole Jijini Dodoma
Baadhi ya watendaji kutoka mamlaka
za Serikali za Mitaa katika sekta ya Afya wa kimfatila WAZIRI wa Nchi,
OfisiyaRais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe.
Selemani Jafo wakati akiwa katika picha na mama aliyejifungua leo
katika kituo cha afya cha Makole Jijini Dodoma
WAZIRI wa Nchi, OfisiyaRais,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo
wakati (kwanza kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mganga Mfawidhi wa
Kituo cha Afya Makole alipofika kuwaona wakina mama waliojifungua leo
kabla ya kutoa mrejesho kwa watanzania mafanikio ya miaka mitano ya
maboresho ya huduma za afya Msingi chini ya Ofisi hiyo kwenye ‘Siku ya
Afya Tamisemi(AFYA DAY)’ iliyofanyika Jijini Dodoma
Baadhi ya watendaji kutoka mamlaka
za Serikali za Mitaa katika sekta ya Afya wa kimfatila WAZIRI wa Nchi,
OfisiyaRais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe.
Selemani Jafo wakati akiwasilisha mrejesho kwa watanzania mafanikio ya
miaka mitano ya maboresho ya huduma za afya Msingi chini ya Ofisi hiyo
kwenye ‘Siku ya Afya Tamisemi(AFYA DAY)’ iliyofanyika Jijini Dodoma
………………………………………………
Na Alex Sonna, Dodoma
Serikali imesema uboreshaji wa
Huduma ya Afya Msingi ni nguzo muhimu katika
kuimarisha uchumi wa kati
kwani uimara wa afya za watanzania ndo chachu ya kuongeza juhudi katika
kufanya kazi ili kuinua uchumi wa taifa.
Kauli hiyo imetolewa leo na
WAZIRI wa Nchi, OfisiyaRais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo wakati akiwasilisha mrejesho kwa
watanzania mafanikio ya miaka mitano ya maboresho ya huduma za afya
Msingi chini ya Ofisi hiyo kwenye ‘Siku ya Afya Tamisemi(AFYA DAY)’
iliyofanyika Jijini Dodoma.
Aidha katika hafla hiyo Waziri
Jafo amejikuta akibubujikwa na machozi namna wananchi walivyo kuwa
wakipata adha na kupoteza maisha kutoka na ukosefu wa huduma za afya
kwenye baadhi ya maeneo nchini jambo lililokuwa linadhohofisha afya za
wananchi katika utafutaji wao kutokana na kutokuwa na afya imara.
Waziri Jafo amesema kwa wananchi
wengi wa likuwa wakipoteza maisha kutokana na kukosa huduma bora za
afya, lakini kwa kipindi cha miaka mitano ya serikali chini ya Rais John
Magufuli imetoa kipaumbele kwa sekta hiyo na kuondoa adha kwa wananchi
hivyo kuchagiza katika utafutaji wa kipato .
“Kuna watu wenye uwezo hawa
fahamu kwamba watanzania walikuwa wanateseka, walikosa kupata huduma
bora za afya, na wanasafiri zaidi ya kilometa 140 kufua tahuduma za
afya, kina mama wanapata matatizo ya fistula, baada ya kupata uchungu
kwa muda mrefu na vituo vipo mbali,” ameeleza Waziri Jafo.
Waziri Jafo ameongezea kuwa Watu
hawafahamu kuna wakina mama wangapi wamekufa kwa kukosa huduma muhimu
wengine wamesafirishwa kwa baiskeli na mikokoteni kufata huduma za
afaya.
Waziri Jafo ameweka wazi kuwa watanzania wanaoishi mijini hawafahamu kama Taifa limepoteza watu wengi kwa kukosa huduma.
“Leo Rais Magufuli amekuja na
maono mapana ya kuhakikisha anaokoa maisha ya watanzania kwa kuwasogezea
hudumaza afya karibu na kutaka watendaji wa huduma za afya kutekeleza
weledi wao kwa ufasaha kwa kutoa huduma bora kwa watanzania wote nchini
bila upendeleo.
Aidha, Waziri Jafo amesema nchi
tangu ilipopata uhuru hadi Rais Magufuli anaingia madarakani kulikuwa
na Hospitali za wilaya 77 katiyaHalmashauri 185.
“Mpaka sasa kwa awamu ya kwanza
hospitali 67 zimekamilika, zikaongezwa zingine na sasa jumla ya
hospitali 99 zinajengwa, hizo za kwanza zimeanza kutoa huduma na hizo
zingine zipo hatua mbalimbali ya ujenzi, tuna kila sababu ya kumshukuru
Rais,”ameeleza Waziri Jafo.
Pia Waziri Jafo amesema zaidi ya zahanati 1198 zimejengwa kwa kipindi cha miaka mitano.
“Niwashukuru wataalam wangu, kwa
kuwa wamekuwa ni injini ya kuhakikisha mambo yanasonga katika sekta ya
afya, idara hii ilikuwa mfu lakini Rais ameibeba idara hii na sasa
inafanyakazi katika ubora unaohitajika na watanzania,”ameshukuru Waziri
Jafo.
Waziri Jafo amebainisha kuwa
wakinamama wajawazito waliojifungua katika vituo hivyo vipya ni 219,764
na waliopata huduma ya upasuaji ni 18,826.
Huku Wagonjwa wengine wakiwemo
kina baba zaidiya 6,000 wamefanyiwa upasuaji wa kawaida kwenye vituo
hivyo, na kina baba wengine wametengeneza familia zao katika vituo
hivyo, wazee zaidi ya 100,000 wamepata huduma,”ameweka bayana Waziri
Jafo.
Lakini pia katika hatua nyingine
Waziri Jafo ametembelea kitu cha afya cha Makole na Kutoa zawadi ya
sabuni, maziwa na maji kwa wakina mama waliojifungua kwa siku ya leo
akiwambia leo ni siku ya Afya TAMISEMI ikionyesha mafanikio
yaliyofanyika ndani ya miaka mitano katika sekta ya afya hapa nchini.
Awali, Mwakilishiwa Katibu Mkuu
Wizara ya Afya, Maendelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk.Grace
Maghembe, amesema kuwa kuna mikoa mitano ili kuwa haina kabisa
hospitali za rufaa za mikoa, lakini kwa sasa zimejengwa na zinatoa
huduma katika ubora wa hali ya juu.
“Uboreshaji wa huduma za afya
ikiwemo za kibingwa nchini umechangia kupunguza idadi ya wagonjwa wa
kupelekwa nje ya nchi”, aesema Maghembe.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu
anayeshughulikia Afya katika Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dk.Dorothy Gwajima
amesema kuwa uwepo wa miundombinu hiyo inatakiwa kwenda sambamba na
utoaji wa huduma bora kwa wananchi ili kuwa vutia watanzania wengi zaidi
kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii iliyoboreshwa(CHF).
No comments:
Post a Comment