Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto-Idara Kuu Afya Edward
Mbanga akiongea na Wauguzi Wakuu wa Wilaya nchini wakati wa ufunguzi wa
kikao kazi cha kuwajengea uwezo wa kusimamia maadili na utendaji kazi
kwenye ukumbi wa Cathedral jijini Dodoma.
Kaimu Katibu Mkuu akiongea na
viongozi hao wakati wa kikao cha mafunzo ambapo aliwataka kuweka
dhamira na malengo ya dhati katika kuboresha maadili katika taaluma ya
uuguzi na ukunga.
Muuguzi Mkuu kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI Charles Kadugushi akitoa salamu kwa washiriki hao
Mgeni rasmi akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wauguzi wakuu wa Wilaya mara baada ya ufunguzi
Picha ya pamoja ya mgeni rasmi na wasajili wa mabaraza ya kitaaluma yaliyopo chini ya wizara ya afya
Mkurugenzi wa Idara ya Uuguzi na Ukunga kutoka Wizara ya Afya Ziana Sellah akiongea wakati wa ufunguzi wa kikao kazi hicho
Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Agnes Mtawa akiwasilisha mada wakati wa kikao kazi hicho kinachofanyika jijini Dodoma.
……………………………………………………………………………
Na.Catherine Sungura,WAMJW-Dodoma
Wauguzi na Wakunga nchini
wametakiwa kusimamia na kutoa huduma kwa kuzingatia miongozo iliyopo na
kwa kutumia utaalamu wao ili kufikia malengo na matumaini ya wateja kwa
weledi mkubwa kwa ajili ya ustawi wa Taifa.
Rai hiyo imetolewa leo na Kaimu
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto –
Idara Kuu Afya Edward Mbanga wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha
kuwajengea uwezo wa kusimamia maadili na utendaji kazi wauguzi wakuu wa
wilaya kinachofanyika jijini hapa.
Bw. Mbanga amesema kuwa wauguzi
na wakunga ndio watendaji wakuu katika vituo vya afya kwenye ngazi ya
jamii hadi Taifa hivyo kuwajibika na utawala bora utaboresha utendaji
pia kuhakikisha kufikia malengo mbalimbali waliyojiwekea katika ngazi
zote.
“Viongozi mnatakiwa kuwa
wabunifu, wachapa kazi, wenye nidhamu na mfano bora wa kuigwa katika
utekelezaji wa majukumu yenu,kwahiyo ni lazima msimamie utoaji wa
huduma uliyo mzuri na wenye heshima na utu.”Alisema
Aidha, Kaimu Katibu Mkuu huyo
aliwakumbusha washiriki hao kuwa katika huduma za uuguzi na ukunga ni
ubinadamu zaidi na kuvaa viatu vya wagonjwa wao “hakuna aliyegongwa
muhuri wa kuugua au kuwa mgonjwa akalazwa ,sisi sote ni wagonjwa
watarajiwa kwahiyo kama ambavyo sisi tungependa kuuguzwa vizuri,kijibiwa
kwa kauli nzuri basi tuhakikishe tunasimamia maadaili ya
kazi”.Alisisitiza Mbanga.
Hatahivyo alisema Serikali
inawahakikishia itaendelea kufanya kazi pamoja na waauguzi kwa kutoa
miongozo thabiti na kuhakikisha upatikanaji wa nyenzo muhimu katika
hospitali na vituo vya kutolea huduma ya afya na kuboresha mazingira ya
kazi yaliyo bora na salama.
Kwa upande wa malalamiko Kaimu
Katibu Mkuu alisema hivi karibuni kumekuwa na malalamko mbalimbali ya
kiutendaji na kitaaluma kutoka kwa wateja wanaofika kupata huduma za
kiafya na hivyo kuleta taswira mbaya kwa taaluma yao na kuonyesha
hakuna usimamizi mzuri wa utoaji huduma za uuguzi na ukunga“tungependa
wateja wetu watoe sifa badala ya malalamiko hivyo kikao hiki mje na
mipango ya kuondokana na malalamiko kwani taaluma yenu ni zaidi taaluma.
Kuhusu suala ya rushwa viongozi
hao wamekumbushwa kuwa mstari wa mbele kupambana na rushwa na
kuhakikisha inatokomezwa katika maeneo yao ya kazi kwani rushwa imekuwa
ikilalamikiwa na kuripotiwa katika kada ya afya nchini.
No comments:
Post a Comment