Profesa
Gerald Misinzo (kulia) akitoa maelekezo kuhusu udhibiti wa panya kwa
kutumia mkojo wa panya katika banda la Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo
(SUA) wakati wa Maoneshoya NaneNane, Viwanja vya Nyakabindi mkoani
Simiyu.
Mtaalam
wa Maabara ya Udongo katika Idara ya Sayansi za Udongo na Jiolojia
(SUA), Stevenson Pelegy akitoa elimu ya jinsi ya kupima udongo kwa
wanafunzi wa Shule ya Sekondari Dutwa, mkoani Simiyu.
Baadhi ya Washiriki kutoka SUA katika Maonesho ya NaneNane mkoani Simiyu wakiwa katika picha ya pamoja katika banda.
Na Mariam Mwayela, Simiyu
NAIBU
Makamu Mkuu wa Utawala wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA),
Prof. Maulid Walad Mwatawala amesema SUaina Mkakati wa kuhakikisha
matokeo ya Tafiti zote zinazofanywa na watafiti zinawafikiakwa wakati.
Akizungumzia
kuhusu maelekezo ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan alipokuwa
akifungua Maonesho ya NaneNane Kitaifa katika viwanja vya Nyakabindi
mkoani Simiyu Prof. Mwatawala alimesema kuwa SUA imeanzisha stashahada
mpya ya Tejnolojia na Uzalishaji wa Mbegu (Diploma in Seed Technology
and Production) ambayo ni maalumu kwa Maafisa Ugani ili kuwaongezea
uwezo katika masuala ya mbegu.
“Stashahada
hii itasaidia Mafisa Ugani kusambaza matokeo ya tafiti mbalimbali kwa
wakulima ili kuweza kusaidia wakulima hao kulima kilimo chenye tija”,
alisema Prof.Mwatawala.
Aidha
aliongeza kuwa mbali na kuanzishwa kwa stashahada hiyo inayotarajiwa
kuanza mwaka huu pia SUA imekuwa ikifanya mafunzo mbalimbali kuhusu
mbegu kwa Maafisa ugani na wakulima kutoka katika Halmashauri na Taasisi
mbalimbali nchini.
“Mpakasasa
Halmashauri na Asasi au Taasisi za binafsi zimekuwa zikileta Maafisa
Ugani na wakulima kwa ajili ya mafunzo mbalimbali juu ya ubebeshaji
miche ya matunda na jinsi ya kusimamia kitalu cha miche na Taasisi ya
Elimu ya Kujiendeleza (ICE) imekuwa ikiandaa mafunzo mbalimbali kutokana
na uhitaji na kwa sasa chuo kiko katika maandalizi ya kuandaa kalenda
ya Mafunzo kwa mwaka mzima itakayokuwa inasambazwa kwa wadau mbalimbali
ili kuweza kuja na kujifunza.” alisema Prof.Mwatawala.
Kuhusu
suala la kutumia kilimo cha kunyunyiza na kuachana na Kilimo cha
umwagiliaji ili kupunguza gharama za kutengeneza miundombinu Prof.
Mwatawala alisema SUA ina Shahada ya Masuala ya usimamiaji wa Rasilimali
Maji hivyo kuna haja ya kuangalia ni namna gani watabadilisha ili
kuweza kusaidia kutoka katika kilimo hicho cha umwagiliaji.
Mapema
juzi mkoani Simiyu Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan aliwaelekeza
watafiti wa Sekta ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi kuhakikisha wanasambaza
matokeo ya tafiti wanazofanya kwa Maafisa Ugani na wadau ili ziweze
kuwafikia wakulima.
“Naelekeza
watafiti watoe matokeo ya tafiti zao kwa maafisa Ugani ili ziweze
kuwafikia wakulima na kunufaika na tafiti hizo,” alisema Mama Samia
Aidha
ameiagiza Wizara ya Kilimo kutoa elimu ya utunzaji na uendeshaji
endelevu wa miundombinu ya umwagiliaji hususan kujikita katika
unyunyizaji na si umwagiliaji ili kupunguza gharama kubwa inayohitajika
katika ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji pamoja na kuelekeza kila
mkoa, wilaya na Halmashauri kutekeleza agizo la kupanda miti na
kuhakikisha inamea.
Chuo
Kikuu cha Sokoine kinashiriki Maonesho ya NaneNane Kanda ya Mashariki
mkoani Morogoro na Kitaifa mkoani Simiyu ambapo Kauli Mbiu ya mwaka huu
ni “Kwa Maendeleo ya Kilimo, Mifugo naUvuvi chagua Viongozi Bora 2020”.
No comments:
Post a Comment