Afisa Mtendaji wa TCCIA Mkoa wa Kilimanjaro Ndugu Boniface Mariki akizungumza kwenye mafunzo ya Vision zero, mafunzo hayo maalumu yaliyoandaliwa na OSHA kwa kushirikiana na TCCIA Mkoa wa Kilimanjaro yaliyofanyika chuo cha VETA Moshi.
Baadhi ya wanachama wa TCCIA mkoa wa Kilimanjaro wakisikiliza maada kwenye ufunguzi wa mafunzo ya Vision zero, mafunzo hayo maalumu yaliyoandaliwa na OSHA kwa kushirikiana na TCCIA Mkoa wa Kilimanjaro yaliyofanyika chuo cha VETA Moshi.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mwangi Rajab Kundya amewataka waajiri mkoani Kilimanjaro kuwekeza kwenye masuala ya usalama na afya kwa wafanyakazi.
Akizungumza Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimnajro kwenye uzinduzi wa Mkakati wa Kupunguza ajali na magonjwa sehemu za kazi, maarafu kama Vision Zero Mjini Moshi, Mhe. Kundya Amesema endapo waajiri watawekeza kwenye masuala ya usalama na Afya, kwa kuweka mikakati endelevu ya kuwalinda wafanyakazi, wataweza kuongeza tija kwenye uzalishaji wao kwenye maeneo ya kazi.
Mkuu huyo wa Wilaya amesema,endapo waajiri watawekeza kwenye masuala ya usalama, uzalishaji utaongeza maradufu na mapato yataongezeka na hivyo kodi pia zitaongezeka na hivyo kuchangia kukuza uchumi wa taifa.
Akiongea kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa OSHA, Mkurugenzi wa Usalama na Afya Mhandisi Alex Ngata,amesema, mafunzo hayo yameandaliwa mahususi kwaajili ya kuwawezesha waajiri nchi, kuhakikisha wanapunguza ama kuondosha kabisa ajali na magonjwa sehemu za kazi.
Mhandisi Ngata amesema mafunzo hayo ambayo tayari yamefanyika katika Mikoa ya Morogoro,Dodoma, Mwanza,Mbeya,Arusha na sasa Kilimnajaro, yatawasaidia waajiri kuweka mikakati madhubuti kwenye maeneo yao kazi, katika kupunguza au kuondoshaa ajali na magonjwa sehemu za kazi.
‘’ Sambamba na mafunzo hayo, vile vile tunapata wasaha wakusikiliza kero na changamoto zao, wakati wa utekelezaji wa sheria na 5 ya mwaka 2003 ya Usalama na Afya, na kuzitatua’’ aliongeza Ndugu Ngata.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Chama cha Wafanyabiashara,Viwanda na Kilimo Nchini (TCCIA) Mkoa wa Kilimanjaro ndugu Boniface Mariki, alisema mafunzo hayo yatawasaidia sana katika utendaji kazi wao, kwani wafanyakazi ni kiungo katika utekelezaji washughuli za viwandani, endapo mfanyakazi ataumia, itakuwa gharama kubwa kiuchumi, kwanza kumtibia na vili vile, shughuli za uzalishaji zitaathirika.
Bwana Mariki amesema wanachama wake wamefurahi kupata mafunzo hayo kwani vision zero ni mpya kwao, na hivyo wameahidi kutekeleza ipasavyo mkakati huo ambao umelenga kupunguza ajali na magonjwa sehemu za kazi, na kuiomba OSHA kuendelea kuwapatia mafunzo kama hayo.
Afisa Mtendaji huyo wa TCCIA amesema endapo waajiri watatenga bajeti zao za utakelezaji wa masuala ya Usalama na Afya kazi zitasaidia sana kuendeleza mipango yao na hivyo kuwa na uhakika wa uzalishaji.
Naye kuwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Tahimini toka toka Mfuko wa Fidia kwa wafanyakazi (WCF) Daktari Abdulsalum Omari amesema, waajiri wanapaswa kufanya tathimini ya hali hatarishi sehemu zao kazi, Amesema waajiri wanatakiwa kutengeneza shabaha ili kutambua una ajali kiasi gani na magonjwa kiasi gani, ili waweze kuweka mifumo ya kudhibiti ajali na magonjwa sehemu za kazi.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Sheria Kutoka OSHA, Bi Joyce Bupe Mwambungu amesema katika mwaka huu wa fedha 2020/2021, wakala umelenga kujenga uelewa zaidi kwa wadau wake masuala mbalimbali ya usalama na afya, ili kututua changamoto wakati wa utekelezaji wa sheria ya Usalama na Afya Mahali Pa kazi.
Bi. Mwambungu amesema, yapo maboresho mengi ambayo OSHA imewayafanya na inaedelea kuyafanya, ili kuweka mazingira mazuri ya ufanyaji biashara kwa wadau, na mpaka sasa Tozo na Ada mbalimbali zilizokuwa zikitozwa zimeondolewa, ili kurahisisha utekelezaji wa sheria.
Akifafanua kuhusiana na TAZO Bi Mwambungu amesema Kwa mwaka huu wa fedha kupitia Bajeti iliyosomwa na waziri wa fedha tumeondoa Tozo ya Elimu kwa Umma, ambayo ilikuwa ikitozwa, hivyo sasa ni fursa kwaajiri kuwasiliana na OSHA kwa kumwandikia Mtedaji Mkuu.
‘’Tozo za mafunzo zipo kisheria zinabaki kama ilivyo, ila tozo ya Elimu kwa Umma ndio imefutwa, hivyo waajiri watapatiwa elimu hiyo bure ambayo ilikuwa ikitozwa endapo OSHA itakuja kukupatia Elimu ’’ aliongeza Mwambungu.
Mafunzo ya Vision zero Mkoani Kilimanjaro yameandaliwa na OSHA kwa kushirikiana na TCCIA Mkoani Kilimanjaro kwa lengo la kuitambulisha Vision zero kwa waajiri na wanachama wa TCCIA mkoa wa Kilimanjaro.
No comments:
Post a Comment