Makamu
wa Rais – Mh. Samia Suluhu akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Afisa Mkuu
wa Fedha Benki ya NMB – Benedicto Baragomwa ni jinsi gani benki hiyo
inavyoisadia sekta ya kilimo nchini, alipotembelea banda lao katika
maonesho ya Nane Nane Mkoani Simiyu. Katika kuendeleza kilimo na
kuwainua wakulima, mwaka huu NMB imetenga TZS bilioni 1.9 zitakazotumika
kwa ajili ya kujenga maghala ya kuifadhia mazao eneo ambalo Serikali
imetenga.
Afisa
Ushirika wa NMB Foundation – Expedito Nyakunga, akitoa maelezo ya namna
ya kumiliki Trekta kwa wananchi waliotembelea banda la NMB kwenye
maonesho ya Nane Nan yanayoendelea katika viwanja vya Nyakabindi mkoani
Simiyu.Wakulima
wakipata elimu ya kibenki na AgriBiashara katika banda la NMB kwenye
maonesho ya Nane Nane katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
No comments:
Post a Comment