Mkurugenzi
wa Mipango, Mikakati na Mahusiano ya Kitaasisi wa TIB, Bw. Patrick
Mongella (kushoto) akizungumza na mmoja wa wateja wa Benki hiyo kutoka
Kampuni ya Mwasonge Farms, Bw. Walter Nyoni (kulia).
Baadhi ya wateja wa Benki ya Maendeleo TIB wanaoshiriki Maonesho ya Nane Nane wakionesha bidhaa wanazozizalisha.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Benki ya Maendeleo TIB wakiwa tayari kuwahudumia
wateja na wananchi wanaotembelea Maonesho ya Nane Nane yanayofanyika
kitaifa katika Viwanja vya Maonesho Nyakabindi vilivyopo mjini Bariadi
mkoani Simiyu.
Benki
ya Maendeleo TIB inashiriki Maonesho ya Nane Nane yanayofanyika kitaifa
katika Viwanja vya Maonesho Nyakabindi vilivyopo mjini Bariadi mkoani
Simiyu.
Benki
ya Maendeleo ya TIB inashiriki maonesho hayo ili kutoa elimu kwa umma,
kutangaza huduma inayozitoa pamoja na kuvutia wateja wapya kwa ajili ya
uwekezaji katika miradi ya kimkakati nchini.
Pia, benki inatumia fursa hiyo kutoa ushuhuda wa miradi ya kimikakati iliyokopeshwa kwa wateja wake waliotapakaa nchi nzima.
No comments:
Post a Comment