Na Mwandishi Wetu
KATIBU
Mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (ALAT)
Elirehema Kaaya amezitaka halmashauri nchini kuhakikisha fedha
zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya
maendeleo zinatumika kikamilifu ikiwa ni pamona na kubana mianya yote ya
ubadhirifu inayoweza kujitokeza.
Amesema
hayo leo jijini Dar es Salaam mara baada ya kukamilisha ziara yake ya
kutembelea baadhi ya miradi inayotekelezwa katika halmashauri mbalimbali
nchini ambapo pamoja na mambo mengine alisisitiza kuwa lengo la
Serikali ni kuona Tanzania nzima inakuwa yenye maendeleo.
Akizungumza
mara baada ya kutembelea miradi shule, zahanati pamoja na vituo vya
afya vilivyopo katika manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam ,amesema ni
vyema halmashauri zinazotekeleza miradi mbalimbali chini, kuhakikisha
zinazingatia suala la matumizi sahihi ya fedha zinazotolewa hatua ambayo
mbali na mambo mengine itawezesha miradi mingine kuendelea kujengwa.
“Serikali
ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli kwa sasa ipo kazini
kuhakikisha miradi yote ya maendeleo inakuwa yenye tija, ili kufanikisha
hilo inatakiwa kuwe na nidhamu nzuri katika matumizi ya fedha za ujenzi
wa miradi ili malengo yote yaliyokusudiwa yaweze kufikiwa” amesema
Kaaya.
Amesema
halmashauri hizo hususani zilizopo katika miji, zina kila sababu ya
kuhakikisha zinafanya matumizi bora ya adhi kwa kujenga majengo hayo ya
ghorofa kwa kuwa kutazifanya halmashauri hizo kuwa na majengo bora na
mengi katika eneo dogo.
Katibu
Mkuu huyo wa ALAT pia amesema halmashauri zote zinazotekeleza ujenzi
wa miradi yake kwa kuzingatia utaratibu huo wa matumizi bora ya ardhi
sambamba na thamani ya fedha katika miradi yake mbalimbali, zinaunga kwa
vitendo harakati za Rais John Magufuli kulieletea Taifa maendeleo.
Aliipongeza
Manispaa ya Ilala kwa utekelezaji mzuri wa miradi ya maendeleo ikiwemo
ya ujenzi wa shule uliozingatia matumizi bora ya ardhi sambamba na
fedha iliyoendana na miradi hiyo jambo lililoiwezesha kupata hati safi.
“Huu
ni mfano mzuri wa matumizi ya fedha hizi za Serikali, lakini pamoja na
hili imekuwa moja ya manispa bora nchini ambazo zimekuwa zikipata hati
safi, hili ni jambo linaloonyesha kuwa ina nidhamu nzuri katika matumizi
ya fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya miradi hiyo” amesema
Kaaya.
Alimaliza
kwa kuzitaka halmashauri zote nchini kuhakikisha inatumia mashine za
kielektroniki (POS) katika utoaji huduma ili kurahisisha kazi ya
ukusanyaji wa mapato mbalimbali ya Serikali.
No comments:
Post a Comment