Msajili wa Bodi ya Usajili Wataalamu wa Mipango Miji Hellen Mtutwa
akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya siku mbili ya Wataalam wa
Mipango Miji nchini tarehe 29 Julai 2020 jijini Dodoma. Wa pili kulia ni
Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Ezekiel Mpanda ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi mafunzo
hayo.Baadhi
ya Washiriki wa mafunzo ya Siku mbili ya Wataalamu wa Mipango Miji
nchini wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa mafunzo
hayo tarehe 29 Julai 2020 jijini Dodoma.Mkurugenzi
wa Sera na Mipango wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Ezekiel Mpanda akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya
siku mbili ya Wtaalam wa Mipango Miji kutoka mikoa ya Tanzania Bara na
Makao makuu iliyofanyika jijini Dodoma tarehe 29 Julai 2020 jijini
Dodoma (PICHA NA WIZARA YA ARDHI)
*******************************
Na Munir Shemweta, WANMM DODOMA
Serikali imewataka
wataalamu wa Mipango Miji nchini kufanya kazi kwa weledi kwa
kuzingatia
taaluma ili kuepukana na malalamiko yanayoendelea kutolewa na jamii
kuhusiana na masuala ya mipango miji.
Kauli hiyo
imetolewa tarehe 29 Julai 2020 jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Sera na
Mipango wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ezekiel Mpanda
kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo Mary Makondo wakati wa ufunguzi
wa mafunzo ya siku mbili kwa wataalam wa Mipango Miji nchini.
Alisema, udhaifu
wa baadhi ya Wataalamu wa Mipango Miji nchini katika kusimamia
utekelezaji wa sheria zilizopo kuhusiana na masuala ya mipango miji
umesababisha baadhi ya miji kutopangika vizuri kama ilivyo kwenye nchi
nyingine duniani na hivyo kuzua malalamiko kutoka kwa wananchi.
’’Napenda kutumia
nafasi hii kuwaasa watumishi wenzangu kufanya kazi kwa uadilifu na kwa
kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utendaji kazi zilizopo’’
alisema Mpanda.
Akigeukia upande
wa Bodi ya Usajili wa Wataalamu wa Miapngo Miji, Mkurugenzi huyo wa Sera
na Mipango aliitaka bodi hiyo kutekeleze majukumu yake ya usimamizi wa
taaluma ipasavyo, ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua stahiki wote
wanaokiuka sheria, kanuni na maadili ya taaluma.
Kwa mujibu wa
Mpanda, kwa muda mrefu sasa imeshuhudiwa malalamiko katika maeneo
mbalimbali nchini kuhusiana na kazi za kimipangomiji hususan
urasimishaji unaoendelea kufanyika nchini na kusisitiza kuwa Wataalam wa
mipangomiji mmeacha jukumu la msingi la kufanya upangaji na badala yake
mmeachia makampuni binafsi pekee kufanya kazi hizo na mbaya zaidi bila
usimamizi madhubuti na kufanya makampuni hayo kupokea fedha nyingi
kutoka kwa wananchi kwa ajili ya kufanya kazi walizoingia mikataba na
Mamlaka za Upangaji lakini hayajakamilisha kazi zao.
Ameshangazwa na
Wataalam wa Mipango Miji kuwaacha wananchi wakivunja sheria za ujenzi
mijini na kueleza kuwa baadhi yao wanafanya hivyo kwa kutojua sheria na
taratibu na kusema kuwa wananchi hao wanahitaji kuelekezwa kwa kuwa
hawafanyi hivyo makusudi.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Makazi Wizara ya Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Deogratius Kalimenze alisema, mafunzo hayo ya siku
mbili ya wataalamu wa Mipango Miji kutoka katika mikoa na makao makuu ya
Wizara yatasaidia kujua changamoto na miongozo ya uaandaji mipango
iliyopitwa na wakati na kuongeza kuwa kwa sasa hapa nchini kumekuwa na
changamoto mbalimbali kama vile mafuriko na kusisitiza kuwa wataalamu
wa mipango miji wanatakiwa kujua namna ya kushiriki kuzitatua changamoto
hizo.
Mwenyekiti wa Bodi
ya Usajili Watraalamu wa Mipango Miji Profesa Wibroad Kombe alisema
bodi yake ina wajibu wa kujenga uwezo kwa wataalamu wa mipango miji ili
kuweza kukabiliana na changamoto za upangaji miji nchini ikiwemo katika
maeneo ya uwekezaji wa ardhi ambapo mipango miji imekuwa sehemu ya
tatizo.
No comments:
Post a Comment