July 1, 2020, Dar es Salaam, Tanzania
Zana hiyo iliyopewa jina la ‘Skills Assessment Tool’ au ‘Zana ya
Tathmini ya Ujuzi’ imeundwa kwa lengo la kuwapunguzia waajiri changamoto
wanazokumbana nazo katika mchakato wa usahili hasa katika kupitia mamia
ya CV wakati wa mchakato wa kuajiri.
Teknolojia ya Skills Assessment Tool inawezesha waajiri kuchuja maombi
ya nafasi ya kazi na kuwawezesha kupata waombaji wachache pekee
waliokidhi vigezo vya kazi husika.
Waombaji watafanyiwa tahmini ya awali katika mchakato wa usahili kupitia
Zana ya Tathmini ya Ujuzi, teknolojia ya tahmini ambayo hupima uwezo wa
waombaji zaidi ya ilivyo kwenye wasifu (CV) zao.
Zana hii huchuja uwezo wa msingi na stadi ngumu zinazohitajika kwa jukumu fulani lililotangazwa.
Matokeo ya tahmini huwasilishwa kwa mwajiri kupitia mfumo wa kufuatilia
waombaji (ATS), dashibodi ya mwajiri ambayo inayomwezesha kuchuja
waajiri bora zaidi kulingana na vigezo tofauti, pamoja na alama za
majaribio.
Akifafanua kuhusu teknolojia hii, Mkurugenzi Mtendaji wa BrighterMonday
Tanzania Reshma Bharmal-Shariff amebainisha namna ambavyo waajiri
wanavyojikuta katika wakati mgumu hasa pale wanapozungukwa na idadi
kubwa ya waombaji wa kazi wasio na sifa stahiki.
“Teknolojia imerahisisha upatikanaji wa taarifa na michakato ya kuomba
ajira, hii imepelekea kwamba mtu yeyote anaweza kuomba kazi yoyote bila
kujali vigezo mahsusi vya kazi husika. Hii inawasababishia maumivu
Maafisa Rasilimali Watu kwani wanajikuta wana CV nyingi za kufanyia
tathmini kabla ya kupata waombaji wachache watakaofaa kwa usahili. "
Alielezea Reshma.
"Hii ndio sababu tuliona haja ya kuwasaidia waajiri kutambua ni mwombaji
gani mwenye ujuzi stahiki wa nafasi hiyo. Mwajiri sio lazima apitie
mamia ya CV tena, kutafuta mwajiri fulani. Waombaji wenye sifa wapo, na
teknolojia hii inampa uwezo mwajiri kumpata mwajiriwa sahihi kwa
kubonyeza vitufe vichache katika kompyuta yake. Kupitia zana hii,
mwajiri anaweza kutazama alama za mwombaji na vigezo vingine kama vile
kiwango cha elimu na uzoefu. Kwa njia hii, mwajiri anaweza kulinganisha
ustadi, sifa, na viwango vya uzoefu kwa muda mfupi",Reshma
Bharmal-Shariff alihitimisha.
Zana hii imeleta ufanisi mkubwa kwa waajiri nchini Tanzania kwani sasa
wanaweza kuchagua waombaji wenye uwezo zaidi bila upendeleo, na kwa
kutumia vigezo vinavyokidhi mahitaji ya mwajiri husika.
No comments:
Post a Comment