Mkurugenzi wa Idara ya Kinga ya
Wizara ya Afya Bw. Leornad Subi akiongea na baadhi ya Wataalam wa Sekta
ya Afya ya Wilaya ya Kahama kabla ya kuanza ukaguzi shirikishi na
watumishi hao katika sekta anwai za hospitali ya Mji Kahama
Mkurugenzi wa Idara ya Kinga ya
Wizara ya Afya Bw. Leornad Subi akiongea na baadhi ya Wataalam wa
hospitali ya kahama mji wakati wa ukaguzi shirikishi na watumishi hao
katika sekta anwai za hospitali ya Mji Kahama.
Wataalam wa masuala ya Kinga
kutoka Wizara ya Afya wakifuatilia Jambo katika hospitali ya kahama mji
wakati wa ukaguzi shirikishi na watumishi hao katika sekta anwai za
hospitali ya Mji Kahama.
Mkurugenzi wa Idara ya Kinga ya
Wizara ya Afya Bw. Leornad Subi akikagua nyaraka ya Vitabu vya Mtua vya
hospitali ya kahama mji wakati wa ukaguzi shirikishi na watumishi hao
katika sekta anwai za hospitali ya Mji Kahama.
…………………………………………………………
Na mwandishi wetu Shinyanga
Tanzania kwa sasa
ni moja ya nchi bora Barani Afrika ambayo imewekeza katika
miundombinu
ya Sekta ya Afya kwa kiwango kikubwa ikiwa ni moja ya mafanikio makubwa
kwa serikali ya wamu ya tano kwa sasa.
Mkurugenzi wa
Kinga kutoka Wizara ya Afya Dkt. Leornad Subi amesema hayo jana
alipofika Wilayani Kahama kufanya ukaguzi shirikishi na kujionea
miundombinu mpya ya Sekta ya Afya Wilayani Kahama.
Dkt. Subi alitaja
lengo la Wizara ya Afya kufanya ukaguzi katika miundombinu ya Afya ni
kuona huduma zinazotolewa katika sekta ya Afya inakizi viwango kwa lengo
la kutoa huduma bora na za uhakika kwa wananchi.
Aidha Dkt. Subi
aliongeza kuwa lengo kubwa la serikali ni kuona kuna ufanisi mkubwa wa
huduma zianzotolewa katika miundombinu hiyo ikiwa ni pamoja na kuongeza
vifaa tiba vitakavyowawezesha wahudumu wa Afya kutoa huduma zenye ubora
ili kuhimarisha Afya za wananchi ikiwemo kupunguza vifo vya mama na
mtoto.
Dkt. Subi
ameongeza kuwa ukaguzi wake katika hospitali ya Mji Kahama amegundua
kuwa kuna mapungufu ya kiutendaji ambayo ni kutoweka vizuri kumbukumbu
katika vitabu vya Mtua kwakuwa kuna masuala ya msingi ambayo wahudumu wa
Afya wameonekana kutoweka kumbukumbu zake kama inavyotakiwa.
Pamoja na kubaini
mapungufu hayo Dkt. Subi amelekeza wataalam wa Afya kuhakikisha
wanafanya ukaguzi wa madawa mara kwa mara na kuwasilisha taarifa ya
ukaguzi huo kwa Mkurugenzi ili kuweza kukabiliana kwa wakati na upungufu
wa vifaa tiba katika hospitali wilayani Kahama.
Aidha ameongeza
kuwa Serikali imekuwa ikitumia rasimali nyingi kuhakikisha kuna
upatikanaji wa dawa za kutosha lakini pia kumekuwepo upotevu wa
dawa unaosababishwa na baadhi ya watumishi wasio kuwa waaminifu kwa
kutofuata mifumo iliyopo au kuweka taarifa vizuri hivyo kuwataka kufanya
ukaguzi wa mara kwa mara na kuweka sawa taarifa ya matumizi ya vifaa
tiba.
Dkt. Subi
ameongeza kuwa kimsingi Idara yake inaangazia sana utoaji elimu ya Afya
kwa wananchi kwani elimu ya Afya ndio msingi wa huduma za kinga hapa
Nchini akitolea mfano Wilaya ya Kahama kuwa na idadi kubwa ya maambukizi
ya ugonjwa wa UKIMWI.
‘’Wilaya ya
Kahama ina jumla ya wagonjwa 15,000 wanaotumia dawa za kupunguza makali
ya UKIMWI idadi hii ni kubwa sana lakini tukitoa elimu ya UKIMWI idadi
hii inaweza kupungua kwa kiasi kikubwa sana na kuokoa fedha nyingi za
serikali zinazotumika kununua dawa za ARV.’’Aliongeza Mkurugenzi Idara
ya Kinga Bw. Leornard Subi.
Pamoja na masuala
mengine yanayoshughulikiwa na idara ya Kinga ya Wizara ya Afya Dkt.
Subi ameongeza kuwa Idara yake pia inashughulikia masuala ya lishe suala
ambalo kimsingi ni la utoaji elimu kwa umma na kuoji kuwa kwanini bado
kuna udumavu katika jamii zetu kwani Tanzania ni Nchi inayozalisha
Chakula cha kutosha na kusema kuwa sio tu watoto wana udumavu wa kimo
pia wanachangamoto ya udumavu wa akili.
Naye Mkurugenzi
wa Mji wa Kahama Bw. Anderson Msumba amesema kuwa kwa upande wake ameona
mapungufu yaliyobainishwa na ukaguzi shirikishi na kuhaidi kuyafanyia
kazi kwa kipindi kifupi yale amabayo hayaitaji fedha laikini pia yale
yanayoitaji rasilimali fedha atayafanyia kazi kabla ya Desemba Mwaka
huu.
Idara ya Kinga ya
Wizara ya Afya inaendelea na kazi ya ukaguzi wa miundombinu ya
Hospitali kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa ambayo ni Shinyanga, Mwanza,
Simiyu, Geita, Mara na Kagera.
No comments:
Post a Comment