katibu Mkuu akiongea na watumishi wa chuo Cha Taifa Cha Sukari kilichopo Kidatu mkoani Morogoro alipotembelea chuo hicho.
3 katibu Mkuu bwana Gerald Kusaya akikagua karakana ya kutengeneza vipuri mbalimbali katika chuo Cha Taifa Cha sukari
3 katibu Mkuu bwana Gerald Kusaya akikagua karakana ya kutengeneza vipuri mbalimbali katika chuo Cha Taifa Cha sukari
………………………………………………………………………………….
Katibu Mkuu Wizara ya
Kilimo Bw.Gerald Kusaya amesema wigo mpana ulipo katika sekta
ya Kilimo
kwenye utunzaji wa mazingira na uendelezaji wa viwanda utumike
kupunguza utegemezi wa Ajira serikalini kwa wahitimu wa vyuo vya Kilimo.
Akiongea leo Mara
alipotembelea chuo Cha Taifa Cha sukari NSI kilichopo Kidatu Kilombero
mkoa wa Morogoro Bw.Kusaya amesema vyuo hivyo vitumie taaluma walizonazo
ikiwemo uzalishaji wa mkaa mbadala na karakana zilizopo kwenye vyuo
vyote vya Kilimo kuongeza taaluma na kuweza kujiajiri pindi wanapohitimu
vyuo hivyo.
Amesema kwa kuwa Kilimo
hakiwezi kutenganishwa na utunzaji wa mazingira na uendelezaji wa
viwanda vidogo ni lazima wanafunzi wanapohitimu katika vyuo vya Kilimo
wawe ni Chachu katika kuendeleza viwanda vidogo na utunzaji wa
mazingira.
Aidha akiongea na
mwanafunzi anayejishughulisha na utengenezaji wa mkaa mbadala Katibu
Mkuu ameahidi kumkutanisha Bi Upendo Emanuel mwanafunzi wa stashahada
katika chuo hicho na wadau mbalimbali wanajishughulisha na utengenezaji
wa bidhaa hiyo ili kuongeza ujuzi.
“Nataka wanafunzi kutoka
vyuo vya Kilimo wawe na wigo mpana wa kujiajiri kwa kuhakikisha
karakana za utengenezaji wa vipuri mbalimbali ambazo zipo katika vyuo
vyetu na taaluma za utunzaji wa mazingira kwa kutengeneza mkaa mbadala
iwe ni Chachu kwa wahitimu kuweza kujiajiri.”Alisema Bw.Kusaya.
Hata hivyo Katibu Mkuu
amesema chuo kishirikiane na viwanda vya sukari na wadau wengine katika
kutatua tatizo la upungufu wa sukari nchini ambalo limekuwa
likijitokeza Mara kwa mara hapa nchini.
“Tuandae mkutano
utakaojumuisha chuo Cha Taifa Cha Sukari wadau wa uzalishaji wa sukari
na wataalamu wengine ili kuhakikisha tatizo hili linakwisha” alisema
Katibu Mkuu.
Katibu Mkuu amemtaka
Mkuu wa chuo hicho Eng.Julius Deteba kuandaa andiko litakalo onesha
mahitaji muhimu ili Wizara iweze kusaidia ujenzi na ukarabati wa
miundombinu na majengo ya chuo hicho.
Aidha Katibu Mkuu
ameshauri Chuo hicho kushirikiana na wadau ili kupata eneo litakalo
tumika kuanzisha shamba darasa la Kilimo Cha miwa.
Akihitimisha kikao chake
na watumishi wa chuo hicho amevitaka vyuo vya Kilimo kujiendesha
kibiashara ili kuweza kutatua changamoto zinazozikumba Taasisi hizo.
No comments:
Post a Comment