Waziri
wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla amesema kuwa Tanzania
iko tayari kupokea watalii kutoka China, India na mataifa mengine ambayo
yameruhusu raia wake kusafiri nje ya nchi zao.
Dkt.
Kigwangalla ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam wakati akizungumza
kwa nyakati tofauti na Balozi wa China nchini Tanzania, Ms.Wng Ke,
Balozi wa India nchini Tanzania, Sanjiv Kohli na Balozi wa Umoja wa
Ulaya nchini Tanzania, Manfredo Fanti.
Akizungumza
na mabalozi hao amesema Tanzania imekwisha fungua anga na kuruhusu
ndege za abiria za kimataifa kutua hali iliyochangia kufunguka kwa Sekta
ya Utalii kutokana na kuwepo kwa utayari, mazingira salama na
maandalizi mazuri ya kupokea na kuhudumia watalii watakaowasili nchini
wakati huu wa janga la Corona.
Dkt.
Kigwangalla amesema ameamua kukutana na kuzungumza na mabalozi hao
kuwaelezea utayari wa Tanzania kupokea watalii na hatua zilizochukuliwa
na Serikali ya Tanzania kufungua Sekta ya Utalii wakati huu wa janga
la Corona.
Aidha,
amesema ameamua kukutana na mabalozi hao kwa kuwa nchi zao zinaleta
watalii wengi Tanzania pia mabalozi hao nafasi kubwa ya ushawishi na
uwezo wa kuwahamasisha mawakala wa Utalii, makampuni ya huduma za
utalii na raia wa nchi zao kufanya safari za kitalii nchini Tanzania.
Amewaeleza
mabalozi hao kuwa Tanzania ilichukua hatua mbalimbali kukabiliana na
janga la Corona ikiwemo uzingatiaji wa masharti na matakwa ya Shirika la
Afya Duniani (WHO) kwa Mamlaka za Afya nchini kuwaelimisha wananchi na
kuwasisitiza kuzingatia kanuni za afya zikiwemo za uvaaji wa barakoa,
matumizi ya vitakasa mikono, unawaji wa mikono mara kwa mara na kuepuka
misongamano hatarishi hali iliyochangia kuwepo kwa maambukizi madogo ya
ugonjwa wa Corona.
Dkt.
Kigwangalla amebainisha kuwa Tanzania haikuchukua hatua kali za
kuwafungia watu majumbani (Lockdown) kama yalivyofanya mataifa mengine
kutokana na uchumi na shughuli za wananchi wengi kutegemea kipato cha
siku kujikimu kimaisha.
Amewaeleza
mabalozi hao kuwa tayari Tanzania imezindundua mwongozo wa Taifa wa
uendeshaji wa Huduma na Biashara ya Utalii ambao kulinda afya na
usalama wa wadau wote wanaojihusisha na biashara ya utalii katika
kipindi hiki cha janga la Corona.
Dkt.
Kigwangalla amewaeleza mabalozi hao kuwa watalii wote wanaowasili
Tanzania katika kipindi hiki cha janga la Corona watakuwa salama
kutokana na uwepo wa mwongozo kwa kuwa huo kwa kuwa unatoa usimamizi
kwenye viwanja vya ndege, hoteli za kitalii, watoa huduma za utalii,
upimaji wa afya za wahudumu na wageni wote wanaoingia nchini pamoja
kukusanya taarifa za wasafiri wote wanaoingia nchini Tanzania.
Dkt.
Kigwangalla amewahakikishia mabalozi hao kuwa mifumo ya huduma za afya
na dharula nchini Tanzania iko tayari kuhudumia watalii watakaokuwa
wakiwasili kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii akibainisha kuwa
Tanzania ina hospitali za kisasa, maabara za upimaji zenye vifaa vyote
vya huduma za dharula katika maeneo tofauti tayari kuhudumia watalii na
wageni watakaoonesha dalili za kuwa na ugonjwa wa Corona.
Pia,
amewaomba mabalozi hao wapange muda wa kutembelea maeneo mbalimbali
yanayotumika kupokelea watalii yakiwemo ya viwanja vya ndege, hoteli za
kitalii na hifadhi mbalimbali ili kujionea utayari wa Tanzania katika
kuwahudumia watalii.
Kwa
upande wao mabalozi hao wakizungumza kwa nyakati tofauti wamemshukuru
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla kwa juhudi
anazozifanya kuhamasisha na kutangaza utalii na kuelezea hatua
zilizochukuliwa na Tanzania kuonesha utayari wake wa kupokea watalii.
Wameipongeza
Serikali kwa kwa juhudi kubwa za kulinda uhifadhi na kuahidi kutoa
ushirikiano katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za uhifadhi.
Mabalozi
hao wamefurahishwa na uwepo wa Mwongozo wa Taifa wa Uendeshaji wa
shughuli za Utalii Tanzania pamoja na kuridhishwa na hali ya utulivu
iliyopo inayowafanya wananchi waendelee na shughuli zao za kila siku.
Aidha,
wameridhishwa na hatua za haraka zilizochukuliwa na Tanzania kufungua
anga jambo lililowezesha mashirika makubwa ya ndege ya kimataifa kuanza
kurejesha safari za anga nchini Tanzania.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment