Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
amesema kuwa, idadi ya wagonjwa wa Corona hapa nchini imepungua kwa
kiasi kikubwa na kubaki na wagonjwa wanne pekee walio katika Mkoa wa Dar
es Salaam.
Waziri Ummy ameyabainisha hayo leo Juni Mosi, 2020, wakati wa ziara ya
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ya uzinduzi wa jengo la Bodi ya Mkonge
lililopewa jina la Mkonge House, na kusisitiza kuwa kwa takwimu hizi
watu wasijisahau, bali waendelee kujikinga na ugonjwa huo.
"Hapa Tanga hatuna mgonjwa wa Corona, DSM katika Hospitali ya Amana
wamebaki 3, Mloganzila 1, Kibaha hatuna mgonjwa, Mwanza hatuna mgonjwa
jambo la kusisitiza ni kuwa Corona bado ipo tuendelee kujikinga, na mimi
nilisema pale Ikulu Dodoma katika Uwaziri wangu sikuwahi kupitia
kipindi kigumu kama hiki cha Corona kwakweli nilihenya" amesema Waziri
Ummy.
Via >> EATV
No comments:
Post a Comment