Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Kabudi akisalimiana na Mkurugenzi
Mkazi wa IMF nchini Tanzania Bw. Jens Reinke
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi
akimuelezea jambo Mkurugenzi Mkazi wa IMF nchini Tanzania Bw. Jens
Reinke leo katika ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkazi wa IMF nchini
Tanzania Bw. Jens Reinke akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi leo
katika ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi akiongea
na Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Nguyen Kim Doanh ambaye amemaliza
muda wake wa utumishi nchini Tanzania
Balozi wa Vietnam nchini, Mhe.
Nguyen Kim Doanh akipokea zawadi kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Kabudi
Balozi wa Vietnam nchini, Mhe.
Nguyen Kim Doanh akimkabidhi zawadi Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Kabudi
*****************************
Shirika la Fedha
Duniani (IMF) limeahidi kuipatia Tanzania fedha itakayoihitaji ili iweze
kuendelea kukabiliana na athari zitokanazo na janga la Covid 19 kwa
ajili ya kuimarisha uchumi wake.
Mkurugenzi Mkazi
wa IMF nchini Tanzania Bw. Jens Reinke ameyasema hayo wakati alipokutana
na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Prof. Palamamba John Kabudi leo katika ofisi ndogo za
wizara jijini Dar es Salaam.
Pia Bw. Reinke
ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hatua
madhubuti inazozichukua katika kukabiliana na janga la Covid 19 ili
kuepusha madhara ya kiuchumi na kijamii.
Mazungumzo hayo
pia yamelenga miradi ya maendeleo, msamaha wa madeni kwa nchi
zinazoendelea ikiwemo Tanzania, ushirikiano baina ya IFM na Tanzania,
biasara na utalii.
Kwa upande wake,
Prof. Kabudi ameishukuru (IMF) kwa msamaha wa madeni ambao umetolewa kwa
Tanzania na nchi nyingine, fedha zitakazoziwezesha nchi hizo kuendelea
kukabiliana na Covid 19.
“Tumeongelea
mambo mbalimbali yanayohusu ushirikiano hasa katika kuimarisha uchumi
wetu baada ya janga la covid 19, usirikiano kati ya Tanzania na IMF
unafahamika na tumekubaliana baadhi ya mambo ambayo tutayafanyia kazi
kwa kina ili tuweze kuimarisha uchumi wetu baada ya corona hasa katika
sekta ya utalii, biashara na miundombinu,” amesema Prof. Kabudi.
Katika hatua
nyingine, Waziri Kabudi amekutana na kumuaga Balozi wa Vietnam nchini,
Mhe. Nguyen Kim Doanh ambaye amemaliza muda wake wa utumishi na
amemtakia maisha mema na kumsihi kuendelea kuwa balozi mwema kwa
Tanzania nchini Vietnam na duniani kwa ujumla.
“Kwa niaba ya
Serikali napenda kukuhakikishia kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na
Vietnam katika nyanja mbalimbali za kimataifa ikiwemo kuiunga mkono
Vietnum katika kugombea nafasi mbalimbali katika Masirika ya KImataifa,”
Amesema Prof. Kabudi
Nae Balozi Doanh
ameishukuru Tanzania kwa ushirikiano ambao imekuwa ikimpatia alipokuwa
akitekeleza majukumu yake nchini wakati wote na kuahidi kuwa ushirikiano
kati ya nchi hizo mbili utaendelea kuimarishwa.
No comments:
Post a Comment