Baadhi ya vibarua/wabeba mizigo
katika bandari ya Bukoba wakiendelea na majumu yao ya kubeba na kupakia
mizigo katika magari ya mizigo.
Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia
Jenerali Marco Elisha Gaguti akiongea na wandesha boda boda wa Manispaa
ya Bukoba akiwaeleza mambo mbalimbali ikiwemo kuchangamkia fursa endapo
meli itakapowasili mjini bukoba na kuanza safari zake za Bukoba –Mwanza.
Baadhi ya waendesha Pikipiki
Manispaa ya Bukoba wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali
Marco Elisha Gaguti katika viwanja vya Gymkhana Mjini Bukoba.
Muonekano wa meli ya NEW MV
VICTORIA HAPA KAZI TU ikiwa katika bandari ya Mwanza tayari kwa kuanza
safari ya majaribio ya kwenda Badari ya Bukoba juni 28,2020.
Mkuu wa mkoa
Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti akionyesha tabasamu
akifurahia kukamilika kwa ukarabati wa meli ya NEW MV VICTORIA HAPA KAZI
TU itakayokuwa ikifanya safari zake kutoka Bukoba kwenda Jijini Mwanza
baada ya Mhe. Rais John Magufuli kuamua meli hiyo ikarabatiwe.
Picha zote na Allawi Kaboyo.
………………………………………………………………………………
Na: Allawi Kaboyo Bukoba.
Wananchi mkoani
Kagera na maeneo jirani watakiwa kujiandaa na fursa mbalimbali
zitakazojitokeza baada ya
meli ya NEW MV VICTORIA HAPA KAZI TU kuanza
safari zake za Bukoba-Mwanaza ikiwa ukarabati wake umekamilika kwa
asilimia 98% huku ikiwa imesimamisha safari hizo kwa takribani Zaidi ya
miaka 3 kutokana na kuharibika.
Akitoa taarifa ya
ujio wa meli hiyo leo Juni 26, 2020 katika mkutano wake na waandishi wa
habari mjini Bukoba, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E.
Gaguti ametoa wito kwa wananchi mkoani humo kujiandaa katika biashara na
safari za kwenda mwanaza kwa kuwa mkombozi sasa anarejea.
Mkuu wa Mkoa
Gaguti amesema kuwa meli hiyo itaanza kufanyiwa majaribio ya safari
ndefu kwa mara ya kwanza ikitokea Jijini Mwanza na kuja bandari ya
Bukoba juni 28,2020 ambapo haitaruhusiwa kubeba abiria Bali itabeba
mizigo zaidi ya tani 100 na kuwataka wananchi wenye mizigo kujitokeza
kwani wakati wa kurudi Mwanza itasafirishwa bure.
“Niombe
kupitia kwenu wanahabari kuwaomba wananchi mkoani hapa kujitokeza kwa
wingi ili kuipokea meli yao inayotarajia kuanza safari yake ya majaribio
siku ya jumapili keshokutwa, ujio wa meli hii ni mapinduzi makubwa ya
usafiri na usafirishaji katika ziwa Victoria chini ya serikali ya awamu
ya tano inayoongozwa na Mhe.Rais John Pombe Magufuli katika kuchochea
uchumi wa wanankagera na watanzania kwaujumla.” Amesema Mkuu wa Mkoa Gaguti.
Baada ya mkutano
huo mkuu wa mkoa wa Kagera amepata fursa ya kuongea na waendesha
pikipiki Maarufu kama (BODA BODA) Manispaa ya Bukoba juu ya ujio wa meli
hiyo ambapo amesema kuwa wao kama wadau wa usafishaji wajiandae
kwaajili ya kufanyakazi ya kuwasafirisha abiria pamoja na mizigo katika
kipindi hiki cha ujio wa meli.
Abdusalum
Mashankala ni mwenyekiti wa waendesha pikipiki manispaa ya Bukoba
amesema ujio wa meli utaongeza mzunguko wa fedha kwa boda boda hao kwa
kuwa watu watakuwa wengi watakao kuwa wanansafiri hivyo amewataka boda
boda wenzake kujiandaa na fursa hiyo ambayo serikali imeamua kuirejesha.
Kwaupande wake
meneja wa mamlaka ya bandari ndg.Bulenge Ndalo amesema mpaka sasa
maandalizi ya kuipokea meli hiyo yanaendelea vizuri ikiwemo kuboresha
miundombinu ya majengo na ofisi pamoja na kujenga godauni la kutunzia
mizigo huku akiwaomba watanzania hasa wanakagera kuja kuwekeza katika
biashara kwenye maeneo ya bandali.
“Nito wito
kwa watanzania kuja kuwekeza kwakuwa tumejenga maeneo ambayo yanaruhusu
kufanyia biashara kama migahawa na sehemu za kuuzia vinywaji hivyo fursa
hii ipo na wakuitumia ni watanzania, kuanza kwa safari za meri kutatoa
ajira hasa kwa vijana na tunatarajia kuanza na vijana 200 watakao kuwa
wakifanya kazi kama vibarua na wafanyakazi wengine kama makarani.” Ameeleza Bw.Ndalo.
Vijana wa kubeba
mizigo ni sehemu ya wadau muhimu katika badari hiyo kwaajili ya kubebea
mizigo wao wamesema kuwa kuanza kwa safari za meli kutachagiza kukua
uchumi wao wa kila siku ambao uliyumba kwa kiasi Fulani meli
iliposimama.
Wameongeza kuwa
baada ya meli kusimama baadhi yao walirudi vijijini lakini sasa
watarejea kuanza kufanyakazi na kujipatia kipato huku wakiomba serikali
kuwawekea utaratibu mzuri wa kuwawezesha kufanyakazi kwa usalama na
Amani.
No comments:
Post a Comment