Taarifa
iliyotolewa na Makao Makuu ya Serikali ya Urusi imesema, Mishustin
alimwambia rais wa nchi hiyo Vladmir Putin kwa njia ya video kuwa,
amepimwa na kukutwa na virusi vya Corona.
Amesema
amejitenga nyumbani kwake na kufuata maelekezo ya madaktari, na
kuongeza kuwa, serikali itaendelea kufanya kazi kama kawaida.
Naibu
wa kwanza wa Waziri Mkuu huyo Andrei Belousov atakaimu kwa muda kazi za
waziri mkuu huyo, kufuatia hatua iliyoidhinishwa na rais Putin.
No comments:
Post a Comment