Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel akieleza jambo
katika sehemu ya kukagua mizigo pindi aliooongozana na Waziri wa
Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla katika uwanja wa ndege wa
KIA.
Waziri wa Maliasili na Utalii
Dkt. Hamisi Kigwangalla na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel
wakisikiliza jambo kutoka kwa Mtaalamu kutoka wakala wa huduma za utalii
nchini wakati wa makabidhiano wa magari hayo manne.
Waziri wa Maliasili na Utalii
Dkt. Hamisi Kigwangalla akiongozana na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin
Mollel pindi walipofanya ziara ya kukagua utayari katika uwanja wa KIA.
Magari
manne yakubeba wagonjwa yaliyotolewa na yametolewa na wakala wa huduma
za utalii kama sehemu ya tahadhari katika kuhakikisha usalama wa Watalii
wataoingia nchini kwaajili ya utalii.
……………………………………..
Na WAMJW- Kilimanjaro
Waziri wa Maliasili na Utalii
Dkt. Hamisi Kigwangalla ameweka wazi kuwa, Tanzania ipo
tayari kupokea
wageni kutoka sehemu yoyote Dunia kwa ajili ya utalii, kufuatia
kuimarisha mifumo ya tahadhari zote za kujikinga dhidi ya maambukizi ya
virusi vya Corona.
Dkt. Kigwangalla ameyasema hayo
leo katika ziara iliyomjumuisha Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel
ikiwa na lengo la kukagua utayari wa nchi katika kudhibiti ugonjwa wa
Corona katika uwanja wa ndege wa KIA na kupokea magari manne ya kubeba
wagonjwa endapo watatokea pindi wawapo nchini kwenye utalii.
Dkt. Kigwangalla amesema kuwa,
Serikali imechukua hatua mbalimbali za kudhibiti maambukizi ya Virusi
vya Corona, ikiwemo kuweka miongozo wakati wa kuingia na kutoka uwanja
wa ndege, muongozo wa namna ya kusafirisha watalii pamoja na muongozo wa
namna ya kuandaa chumba cha wageni
“Katika kipindi hiki cha mlipuko
wa ugonjwa wa Corona Duniani, tumeweka miongozo kwa pale uwanja wa
ndege, tumeweka muongozo wakati wa kuingia na kutoka tumeweka muongozo
namna ya kusafisha Watalii kutoka uwanja wa ndege mpaka hotelini,
tumeweka muongozo namna ya kuandaa chumba cha mgeni, namna ya kuandaa
chakula, kila kitu tumeweka muongozo ” alisema
Aliendelea kusema kuwa, Serikali
imechagua baadhi ya vituo vya Afya mahususi kwa ajili ya watalii Mkoani
Arusha, Serengeti na Ngorongoro lengo ni kuthibitisha usalama wa afya ya
Watalii waingiapo nchini.
Naye Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel amesema
kuwa, Serikali imepokea magari manne ya kubeba wagonjwa(ambulance)
yaliyokidhi miongozo ambayo yametolewa na wakala wa huduma za utalii
nchini ikiwa ni sehemu ya tahadhari katika kuhakikisha usalama wa
Watalii wataoingia nchini.
“Tumeona magari ambayo
yamezingatia zile taratibu na miongozo yote ambayo inatakiwa kuhakikisha
Watalii wetu wapo salama na endapo kutakuwa na tatizo litaweza fanyiwa
utatuzi mara moja ” alisema Dkt. Mollel.
Aidha, alisema kuwa, katika
kuboresha tahadhari zaidi magari yaliyotolewa yanalenga kuwakinga
madereva na Watalii kwa kutenganishwa kwa kioo ili kudhibiti mnyororo wa
maambukizi ya virusi vya Corona endapo atatokea.
“Magari yenyewe yatakuwa Dereva
anaingia ndani, lakini kunakuwa na kinga inayowatenganisha Watalii na
madereva wetu jambo litalosaidia kudhibiti maambukizi endapo yatatokea ”
alisema.
No comments:
Post a Comment