
Afisa-ustawi-wilaya-ya-kaskazini-A-Unguja-Khamis-Kona-akisisitiza-jambo
……………………………………………………………….
Na Masanja Mabula –Zanzibar.
JUMLA ya kesi 42 za matukio ya
udhalilishaji kwa wanawake na watoto zimeripotiwa katika dawati la
jinsia mkoa wa kaskazini Unguja kutoka mwezi Januari hadi mei mwaka
2020.
Akiwasilisha ripoti juu ya matukio
hayo mkuu wa dawati la jinsia mkoa wa kaskazini Unguja
Fatma Juma
Mahmoud alisema matukio hayo yamefanyika katika wilaya zote mbili za
mkoa huo ambapo wilaya ya kaskazini A kumefanyika matukio 19 huku
kaskazini B kumefanyika matukio 23.
Alisema idadi kubwa ya kesi hizo
zipo katika hali ya upelelezi hadi sasa kwa lengo la kubaini ukweli juu
ya watu wanaotuhimiwa kufanya matukio hayo.
Pia afisa huyo alisema kesi
nyengine (2) hadi sasa zipo ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka (DPP)
zikisubiri kufikishwa Mahamakamani.
Kuhusu kesi ambayo ipo Mahakamani
hadi sasa alisema ni kesi (1)Mahakamani moja na kwamba kesi hio imesita
kuendelea kuskilizwa kwa kile alichokisema uwepo wa maaradhi ya korona
ambapo Mahakama zimestisha shughuli za usikilizaji wa baadhi ya kesi.
Aidha mkuu huyo wa dawati la
jinsia alisema wamekua wakikabiliana na changamoto mbali mbali ikiwemo
muhali kwa baadhi ya wanajamii jambo ambalo alisema linarudisha nyuma.
Kwa upande wake afisa dawati la
jinsia wilaya ya kaskazini A Unguja Khamis Kona Khamis alisema kuendelea
kuwepo kwa matukio hayo katika wilaya na mkoa huo kunachangiwa na
sababu mbali mbali.
Akitaja baadhi ya sababu hizo alisema ni ucheleweshaji wa uandaaji wa kesi kabla kufikishwa Mahakamani.
‘’Mazingira ya aina hii hupelekea
watu kukaa pembeni na kusuluhishana mwisho wa siku kesi haziendi
Mahamani na hata zikienda hua hazina nguvu kwa kuwa wahusika hushindwa
kutoa ushahidi’’aliongezea.
Hata hivyo alisema katika wilaya
yake kumeibuka chanagmoto nyengine ya utekelezwaji wa watoto ambao
wazazi huachana na kupelekea watoto kuhangaika hatimae kujikuta
wamefanyiwa vitendo viovu.
Kwa upad wake mratibu wa dawati la
jinsia katika mkoa huo Suleiman Juma alisema jeshi la polisi
wanakabiliana na hali ngumu katika mapambano hayo.
Alisema kucheleweshwa kwa majalada
ndani ya ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka kunawapa mwanya mkubwa
wahusika kukaa pemeni na kusuluhishana.
Alisema wakati wote huo hawawezi
kukaa na mtuhumiwa ndani ya kituo cha polisi bali mtuhumiwa hutakiwa
kuripoti kila baada ya muda lakini mara moja hupewa taarifa kuwa
wahusika wameshaoana hivyo hawataki tena kesi.
Alieleza kuwa kwa mazingira hayo
matendo ya udhalilishaji kwa wanawake na watoto hayataweza kumalizika
bila ya jamii kukubali kubadilika.
Meneja wa miradi kutoka
Tamwa-Zanzibar Asha Abdi alisema jamii ina haja ya kubadilika na kurudi
kwenye malezi ya zamani ikiwemo kuwaadhibu watoto wao pale wanapokosea.
Hata hivyo alisema kuna haja kubwa
ya kufanyiwa marekebisho kwa baadhi ya sharia ambazo bado zinaonekana
kuwa changamoto dhidi ya mapambano ya udhalilishaji kwa wanawake na
watoto.
No comments:
Post a Comment