Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji na Usafi
wa Mazingira katika mji wa Kahama na Shinyanga (Kahama Shinyanga Water
Supply and Sanitation Authority(KASHWASA) inavyozalisha na kusambaza
maji katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania, Mhandisi Joshua Mgeyekwa
akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko mapipa 20
yenye ujazo wa lita 210 kila moja kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za
serikali katika mapambano dhidi ya Virusi Vya Corona ‘Covid – 19’ kwenye
maeneo huduma za kijamii katika wilaya ya Shinyanga leo Alhamis Aprili
30,2020. Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kulia)
akijaribu kufungua koki ya moja ya mapipa 20 yenye ujazo lita 210 kila
moja yaliyotolewa na KASHWASA kwa ajili ya kuunga juhudi za serikali
katika mapambano dhidi ya Virusi Vya Corona ‘Covid – 19’ kwenye maeneo
huduma za kijamii katika wilaya ya Shinyanga. Kushoto ni Mkurugenzi
Mtendaji wa KASHWASA Mhandisi Joshua Mgeyekwa.
Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko
akizungumza wakati wa kupokea mchango wa mapipa 20 yaliyotolewa na
KASHWASA kwa ajili kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya Corona katika
wilaya ya Shinyanga. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa KASHWASA
Mhandisi Joshua Mgeyekwa.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko
akiishukuru KASHWASA kwa mchango wa mapipa 20 kwa ajili kukabiliana na
Maambukizi ya Virusi vya Corona katika wilaya ya Shinyanga ambapo
alisema mapipa hayo yatapelekwa katika halmashauri ya wilaya ya
Shinyanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa KASHWASA
Mhandisi Joshua Mgeyekwa akizungumza wakati akimkabidhi Mkuu wa wilaya
ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kulia) mapipa 20 kwa ajili ya kuunga
juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya Virusi Vya Corona ‘Covid –
19’ katika wilaya ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe.
Jasinta Mboneko (katikati) akimkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya
wilaya ya Shinyanga Mhe. Hoja Mahiba (kulia) mapipa 20 yaliyotolewa na
KASHWASA ili yakatumike kwenye maeneo yenye huduma za kijamii katika
halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa
KASHWASA Mhandisi Joshua Mgeyekwa.
Muonekano wa mapipa yaliyotolewa na KASHWASA kwa ajili ya mapambano dhidi ya Virusi vya Corona katika wilaya ya Shinyanga.
Picha ya pamoja baada ya
makabidhiano ya mapipa 20 yaliyotolewa na KASHWASA kwa ajili ya kuunga
juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya Virusi Vya Corona ‘Covid –
19’ katika wilaya ya Shinyanga.
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mamlaka
ya Maji na Usafi wa Mazingira katika mji wa Kahama na Shinyanga (Kahama
Shinyanga Water Supply and Sanitation Authority(KASHWASA) inavyozalisha
na kusambaza maji nchini imetoa msaada wa mapipa 20 yenye ujazo wa lita
210 kila moja kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za serikali katika
mapambano dhidi ya Virusi Vya Corona ‘Covid – 19’ kwenye maeneo huduma
za kijamii katika wilaya ya Shinyanga.
Mapipa
hayo yamekabidhiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa KASHWASA Mhandisi Joshua
Mgeyekwa kwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko leo
Alhamis Aprili 30,2020.
Mhandisi
Mgeyekwa amesema KASHWASA itaendelea kushirikiana na serikaliH katika
mapambano dhidi ya Virusi vya Corona kwani Corona inaweza kuathiri
shughuli za kijamii na kiuchumi.
“Tumekabidhi mapipa 20 yenye
ujazo wa lita 210 kila moja jumla lita 4,200 ambayo yatawekwa kwenye
maeneo ya watu wengi katika wilaya ya Shinyanga kwa ajili ya kukabiliana
na maambukizi ya Virusi vya Corona”,amesema Mhandisi Mgeyekwa
“Katika kuunga mkono juhudi
za serikali kwenye mapambano dhidi ya Corona, KASHWASA imechangia mapipa
140 yenye thamani ya shilingi Milioni 11.8 kwa ajili ya wilaya 8 za
mikoa ya Shinyanga,Mwanza na Tabora ambako KASHWASA inafanya kazi zake
ambapo kati ya mapipa hayo 140, 20 ni kwa ajili ya wilaya ya Shinyanga”,ameeleza Mhandisi Mgeyekwa.
Akipokea Mapipa hayo, Mkuu wa
Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko ameishukuru KASHWASA kwa
mchango huo akibainisha kwa utasaidia kuongeza nguvu katika mapambano
dhidi ya Virusi vya Corona.
“Kwa niaba ya wananchi wa
wilaya ya Shinyanga ninawashukuru sana KASHWASA kwa kutupatia mapipa
haya. Tutayapeleka katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ili
yakatumike kwenye maeneo ambayo yana mikusanyiko ya watu wengi ikiwemo
minada na masoko”,amesema Mhe. Mboneko.
“Mkurugenzi wa halmashauri na
watendaji wengine hakikisheni mapipa/madumu haya yanakuwa masafi na
yawe na maji muda. Simamieni pia wananchi wasiweke ndoo tupu bila maji
na wanawe kwa maji na sabuni muda wote”,ameongeza Mboneko.
Aidha amesema serikali
inaendelea kutoa elimu kuhusu Corona kwa njia mbalimbali huku
akiwasisitiza wazazi na walezi kuzuia watoto wasizurure mtaani watulie
nyumbani na wafanyabiashara wasipandishe bei ya vifaa vinavyotumika
katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona.
Naye Mkurugenzi wa
Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Hoja Mahiba ameahidi kutunza
mapipa hayo na kwamba yatawekwa kwenye maeneo yenye huduma za kijamii
ikiwemo minada,masoko,zahanati na vituo vya afya.
No comments:
Post a Comment