Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Utangazaji Tanzania (TBC), Dkt. Ayoub Rioba akisoma taarifa ya ujenzi wa
jengo la televisheni kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya
utangazaji mbele ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt.
Harrison Mwakyembe lililotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Korea ambapo
amesema kwa sasa jengo hilo ujenzi wake umefikia 20%.
Waziri wa Habari Dkt. Harrison
Mwakyembe (katikati) akikata utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi
la ujenzi wa studio ya televisheni ya Taifa (TBC) kwa ajili ya
uboreshaji wa mundombinu ya utangazaji. Kushoto ni Katibu Mkuu Habari,
Dkt. Hassan Abbasi na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji
Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba.
Waziri wa Habari, Dkt.Mwakyembe
akiweka tofali kama ishara ya kuanza ujenzi wa studio za televisheni kwa
ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya utangazaji ya Shirika la
Utangazaji Tanzania (TBC). Jengo hilo linajengwa kwenye ofisi za TBC
zilizopo Mikocheni Dar es salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo, Dkt. Harrrison Mwakyembe, Katibu Mkuu Habari Dkt. Hassan
Abbasi na Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub
Rioba wakiwa kwenye picha ya pamoja na wasimamizi wa mradi wa ujenzi wa
jengo la televisheni ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) baada ya
kuweka jiwe la msingi la kuanza rasmi ujenzi wa jingo hilo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo, Dkt. Harrrison Mwakyembe, Katibu Mkuu Habari Dkt. Hassan
Abbasi na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt.
Ayub Rioba wakiwa kwenye picha ya pamoja na meneja pamoja na wakurugenzi
wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), baada ya kuweka jiwe la msingi
la kuanza rasmi ujenzi wa jengo la studio la Shirika la Utangazaji
Tanzania (TBC).
Katibu Mkuu Habari, Dkt. Hassan
Abbasi akiongea wakati wa hafla hiyo ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi
wa studio mpya ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) inayojengwa
katika eneo la ofisi hizo zilizopo Mikocheni. Programu Tumizi (App) ya
Safari Channel, pamoja na mfumo mpya wa upashanaji habari unaofahamika
kama TBC Aridhio. Hafla hiyo ilifanyika tarehe 30 Machi,2020.
Mkurugenzi wa Shirika la
Utangazaji Tanzania (TBC) akizungumza wakati wa hafla hiyo ya uwekaji
jiwe la msingi la ujenzi wa studio mpya ya Shirika la Utangazaji
Tanzania (TBC) inayojengwa katika eneo la ofisi hizo zilizopo Mikocheni.
Programu Tumizi (App) ya Safari Channel, pamoja na mfumo mpya wa
upashanaji habari unaofahamika kama TBC Aridhio. Hafla hiyo ilifanyika
tarehe 30 Machi,2020.
Mwalimu wa Kiswahili Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam, Elizabeth Mahenge akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
Elizabeth Mahenge ndiye aliyekuja na neno ARIDHIO ambapo amesema neno
ARIDHIO ni kisawe cha neno taarifa na pia ni kisawe cha neno Habari.
Msanii Mrisho Mpoti akitoa
burudani wakati wa uzinduzi huo uliofanyika kwenye makao makuu ya
Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) zilizoko Mikocheni jijini Dar es
salaam
Waziri wa Habari, Dkt. Harrison
Mwakyembe akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi rasmi wa Programu Tumizi
(app) maalumu ya Chaneli ya Safari itakayokuwa ikipatikana kupitia
playstore na IOS.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe,akizungumza wakati wa hafla hiyo
ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa studio mpya ya Shirika la
Utangazaji Tanzania (TBC) inayojengwa katika eneo la ofisi hizo zilizopo
Mikocheni. Programu Tumizi (App) ya Safari Channel, pamoja na mfumo
mpya wa upashanaji habari unaofahamika kama TBC Aridhio. Hafla hiyo
ilifanyika tarehe 30 Machi,2020.
………………………………………………………………………………………………
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka watangazaji na watumishi
wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kudumisha weledi na kujituma ili
wengine wapate kuiga mambo mazuri kutoka kwao.
Ameyasema hayo jijini Dar es
Salaam, wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa studio
mpya ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) inayojengwa katika eneo la
ofisi hizo zilizopo Mikocheni. Aidha Dkt. Mwakyembe alizindua Programu
Tumizi (App) ya Safari Channel, pamoja na mfumo mpya wa upashanaji
habari unaofahamika kama TBC Aridhio ambapo neno Aridhio linamaanisha taarifa au habari.
“Tuna deni kubwa la
kuhakikisha tunadumisha weledi na kujituma hivyo kuendelea kuwa kiongozi
wa habari hapa nchini, lazima TBC kiwe ni chombo cha rejea,wakitangaza
wengine mtu awe na shauku ya kujua TBC imesema nini kwanza”,amesema
Dkt.Mwakyembe.
Kwa upande wake, katibu Mkuu
wa Wizara ya habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi
amewapongeza wafanyakazi wa shirika hilo kwa hatua hiyo kubwa ya kuleta
mapinduzi na ubunifu katika tasnia ya habari katika chaneli hiyo ya ya
Tanzania inayotegemewa na taifa.
Mabadiliko haya makubwa ya
upashanaji habari ndani ya TBC yanakuja baada ya miaka 13, ambapo
safari hii ilianza mwaka 2007. Ujenzi wa jengo hilo la kisasa umeanza
Februari, 2020 na utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 2.38/- na
unatarajiwa kukamilika Agosti 2020, ambapo hadi sasa ujenzi huo umefikia
asilimia 20.
Akizungumza wakati wa uzinduzi
wa mfumo huo mpya wa upashanaji habari Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayoub Rioba amesema kuwa kutokana na
mahitaji ya sasa ya dunia ya sayansi na teknolojia imelazimika mifumo ya
zamani ya upashanaji habari kupinduliwa na kuja na namna mpya za
upashanaji habari. Aidha Dkt. Ayoub Rioba ameishukuru Wizara kwa namna
ambavyo imekuwa bega kwa bega katika kuunga mkono mafanikio ya Shirika
hilo.
No comments:
Post a Comment