Pages

Tuesday, March 3, 2020

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA MHE KHAMIS JUMA MWALIM AMEWATAKA WAAJIRI WA SEKTA BINAFSI, SERIKALI NA WAJASIRIAMALI KUJIUNGA NA MFUKO WA HIFADHI YA JAMII ZSSF ILI KUPATA MAFAO WAKATI WA KUSTAAFU


news phpto

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA MHE KHAMIS JUMA MWALIM AMEWATAKA WAAJIRI WA SEKTA BINAFSI, SERIKALI NA WAJASIRIAMALI KUJIUNGA NA MFUKO WA HIFADHI YA JAMII ZSSF ILI KUPATA MAFAO WAKATI WA KUSTAAFU.


WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA MHE KHAMIS JUMA MWALIM AMEWATAKA WAAJIRI WA SEKTA BINAFSI, SERIKALI NA WAJASIRIAMALI KUJIUNGA NA MFUKO WA HIFADHI YA JAMII ZSSF ILI KUPATA MAFAO WAKATI WA KUSTAAFU.

AKIFUNGUA MKUTANO WA TANO WA WADAU WA MFUKO HUO KATIKA UKUMBI WA ZSSF KARIAKOO AMESEMA HATUA HIYO ITASAIDIA KUIMARIKA KWA UCHUMI WAO KWA KUPATA FEDHA ZA KUJIENDELEZA NA MAISHA YA BAADAE.

AMESEMA ZSSF IMEANZISHWA KWA AJILI YA KUWASAIDIA WANANCHI HIVYO NI VYEMA JAMII KUSHIRIKIANA NA MFUKO HUO KATIKA KUHAKIKISHA WANAJIUNGA NA KULIPA MICHANGO KWA WAKATI.

AKIELEZEA LENGO LA MKUTANO HUO MKURUGENZI MTENDAJI WA MFUKO WA HIFADHI YA JAMII ZSSF BI SABRA ISSA MACHANO AMESEMA NI KUWAPA TAARIFA WADAU ILI WAWEZE KUFAHAMU MAENDELEO NA MATATIZO YANAYOUKABILI MFUKO HUO.

NAO WASHIRIKI WA MKUTANO HUO WAMEUOMBA UONGOZI WA ZSSF KUFANYA HARAKA KATIKA KULIPA MAFAO YA WASTAAFU ILI WAWEZE KUJIPANGA KATIKA KUJIENDELEZA KIMAISHA.

MADA MBALIMBALI ZIMEJADILIWA KATIKA MKUTANO HUO IKIWEMO UWEKEZAJI NA UENDESHAJI WA ZSSF, MFUKO WA UCHANGIAJI WA HIARI NA AFYA NJEMA KWA WAFANYAKAZI NA WASTAAFU.

No comments:

Post a Comment