Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Omari
Mgumba akikagua bidhaa za sola power kutoka kampuni ya Poa Portable
Power wakati wa kongamano la vijana lililofanyika Mkoani Arusha katika
ukumbi wa Golden Rose hivi karibuni kushoto ni muoneshaji bwana Emanuel
Godwin wa kampuni hiyo.
Naibu Waziri Kilimo Mhe. Omari Mgumba akihutubia vijana wakulima wakati wa kongamano la vijana mkoani Arusha hiv karibuni
Vijana walioshiriki aktika Kongamano la vijana wakiwa ukumbini
………………………………………………………………………………………………
Na Bashiri Saluma Arusha
Serikali imewataka wahitimu wa
vyuo vya kilimo kote nchini kutumia fursa ya uhaba wa
maafisa ugani
ulioko nchini kwa kwenda kutoa elimu kwa wakulima na kuanzisha mashamba
ya mfano kwa wakulima
Akiongea wakati wa ufunguzi wa
kongamano la vijana wakulima mkoani Arusha uliofanyika katika Ukumbi wa
Hoteli ya Golden Rose Naibu Waziri Kilimo Mhe. Omari Mgumba amesema
kwamba maafisa ugani wafungue mashamba ya mfano na watoe huduma kwa
wakulima kama sehemu ya kujiajiri .
“Sasa hivi kilimo
kimebadilika wapo watu ambao wanazunguka kuwatafuta wataalamu wa kilimo
ili wakapate huduma kwenye shughuli zao na wapo tayari kulipia
wataalamu lakini wagani hawapatikani. Alisema Mhe Omari Mgumba.
Amewataka vijana kuwekeza kwenye Uzalishaji wa mbegu bora za mazao nchini kwani kuna uhitaji mkubwa wa mbegu nchini.
Akitolea mfano amebainisha
kwamba mahitaji ya mbegu ni tani 187,000 kwa mwaka wakati uzalishaji wa
ndani ni tani 71,000 hivyo amewataka vijana kutumia fursa hiyo
kuwekeza kwenye uzalishaji wa mbegu hasa za mazao ya bustani na maua
katika ukanda huuwa kaskazini ambao unajumuisha mikoa ya
Arusha,Tanga,Kilimanjaro na Manyara.
Hata hivyo amebainisha kwamba
jumla ya vijana hapa nchini ni milioni 16.1 sawa na asilimia 35 ya
idadi ya watu wote, Kwa mujibu wa Utafiti wa Nguvu Kazi ya Taifa wa
mwaka 2014, nguvu kazi ya vijana ni asilimia 67.1 ya nguvu kazi yote ya
Taifa na kiwango cha ukosefu wa ajira ni asilimia 11.7 ya nguvu kazi
yote.
“ Takwimu hizi zinaonesha umuhimu wa Nguvu Kazi ya Vijana na Sekta ya Kilimo kwa maendeleo ya Taifa” Alibainisha Mhe Mgumba.
Aidha amesema kilimo ndio
sekta pekee ambayo haibagui mtu aliyesoma na asiyesoma kwani kilimo
kinahitaji elimu kidogo sana na unapata utajiri kupitia kilimo
alisisitiza Mhe. Mgumba
Serikali kupitia Wizara ya
Kilimo inatekeleza Mkakati wa Miaka Mitano wa Taifa kwa Vijana kushiriki
katika sekta ya kilimo wa mwaka 2016/17 hadi 2020/21. Utekelezaji wa
Mkakati huo unahusu masuala ya ardhi ya kilimo, rasilimali fedha kwa
ajili ya kilimo, pembejeo na zana za kilimo, masoko ya mazao ya kilimo,
mabadiliko ya tabianchi, ujasiliamali .
Hata hivyo alibainisha kwamba
Serikali inaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa vijana ambapo tayari
inatekeleza Mkakati wa Kupunguza Upotevu wa Mazao Baada ya Kuvunwa na
takwimu zinaonesha upotevu wa mazao yasiyo ya nafaka ni asilimia kati ya
30-40 ili kupunguza hasara kwa mkulima.
Aidha, Naibu Waziri amefafanua
kwamba Wizara ya Kilimo kupitia TPRI itaendelea kutoa mafunzo ya
matumizi bora ya viuatilifu kwa wakulima na wafanyabiashara nchi nzima
ili kuhakikisha matumizi bora ya viuatilifu na afya ya mimea ili
kumsaidia mkulima.
“TPRI imeendelea kusajili
viuatilifu, kufanya ukaguzi wa pembejeo zisizofaa kwa matumizi ya kilimo
kwa wafanyabiashara wasiowaaminifu na kutoa elimu kwa wakulima ili
wasipate hasara za kutumia viuatilifu visivyo na ubora” Amesema Mhe. Mgumba
No comments:
Post a Comment