Pages

Monday, March 2, 2020

Ufunguzi wa mafunzo ya siku 12 ya Ukandarsa kwa Kutumia Teknolojia ya Stahiki Mkoani Morogoro



Mkurugenzi wa utawala na rasilimali watu wizara ya ujenzi Ziana Mlawa (Katikati)akiwataka wanawake kuchangamukia fursa za ujenzi wa matengenezo ya barabara wakati wa kufungua mafunzo ya siku 12 yaliyofanyika mkoani Morogoro ambayo ni mafunzo ya hatua za awali  za ukandarasi kwa kutumia teknolojia stahiki na nguvu kazi .
Washiriki hao wa mafunzo  ya wanawake katika kutekeleza ukandarasi kwa kutumia teknolojia na nguvu kazi yaliyofanyika chuo  cha ujenzi mkoani Morogoro wakitazama na kufatilia kwa makini ushauri wa Mkurugenzi wa utawala na rasilimali watu wizara ya ujenzi Ziana Mlawa.
Mratibu wa kitengo cha ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara mhandisi Gradness Kitaly akitoa taarifa ya mafuzo kwa mgeni rasmi Ziana Mlawa na changamoto zinazowakabili wanawake katika kujisajiri ili kutekeleza shughuli za ujenzi na matengenezo ya  barabara .
Wanawake kutoka mikoa nane hapa nchini  waliohudhuria mafunzo  ya ukandarasi kwa kutumia teknolojia stahiki na nguvu kazi mkoani Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Ziana Mlawa (watatu kutoka kulia ) akifatiwa na mkuu wa chuo cha ujenzi Mkoani Morogoro  Mlyapali.
Wanawake waliohudhuria mafunzo ya  ya awali ya ukandarasi  kwa kutumia teknolojia stahiki na nguvu kazi  yaliyofanyika mkoani Morogoro wakifatilia kwa makini maelekezo ya mgeni rasmi ambaye pia ni Mkurugenzi wa utawala na rasilimali watu wizara ya ujenzi Ziana Mlawa (hayupo kweye picha).

No comments:

Post a Comment