************************
WAZIRI MKUU
Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kufanya kazi kwa
kushirikiana
na wawekezaji katika sekta mbalimbali nchini wakiwemo wenye
viwanda vya kuzalisha saruji.
Amesema katika
kuhakikisha inalinda viwanda vya ndani vya kuzalisha saruji Serikali
imeamua kuzuia uingizwaji wa saruji kutoka nje ya nchi.
Waziri Mkuu
aliyasema hayo leo(Jumanne, Machi 3, 2020) wakati akizungumza na
watumishi wa kiwanda cha saruji cha Simba alipotembelea kiwanda hicho
akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Tanga.
Amesema licha ya
Serikali kupata kodi kutokana na uwepo wa kiwanda hicho, pia kimesaidia
katika kutatua changamoto ya ajira hususani kwa vijana.
Naye, Waziri wa
Madini, Doto Biteko amesema ameupongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa
kuwa wanazingatia sheria zote za madini ukilinganisha na viwanda
vingine.
Awali, Mkurugenzi
Mtendaji wa kiwanda hicho, Reinhardt Swart alisema kiwanda hicho
kinauwezo wa kuzalisha tani milioni 1.25 kwa mwaka lakini kutokana na
mahitaji ya soko kinazalisha tani milioni 1.075 kwa mwaka.
Mkurugenzi huyo
aliongeza kuwa kiwanda hicho kimeajiri jumla ya wafanyakazi 319 kati yao
wazawa ni 316 na watumishi watatu ni raia ya kigeni.
Pia, Mkurugenzi
huyo alitumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya Awamu ya Tano
inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli kwa kuboresha mazingira ya
uwekezaji nchini.
No comments:
Post a Comment