Rais
wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza masharti zaidi ya kukabiliana na
kuenea kwa virusi vya corona wiki mbili baada ya kupiga marufuku usafiri
wa Umma.
Katika
hotuba yake kwa taifa iliyopeperushwa moja kwa moja kwenye televisheni
usiku wa Jumatatu ,Museveni amepiga marufuku usafiri wa kutumia magari
binafsi na boda boda kuanzia saa nne usiku.
Mtu
yeyote anayehitaji huduma za dharura za kiafya kama vile kujifungua au
kufanyiwa upasuaji anatakiwa kupata idhini kutoka kwa maafisa wa
serikali katika ngazi ya Wilaya kabla ya kutoka nyumbani
Wauzaji
bidhaa za chakula sokoni watahitajika kuondoka maeneo yao ya biashara
hadi pale serikali itakapokamilisha kushughulikia maeneo mapya ya wao
kuuzia bidhaa zao .
Rais
Museveni pia ameahidi msaada wa chakula kwa watu ambao hawafanyi kazi
kutokana na vikwazo vya kukabiliana na covid-19 na hawana uwezo wa
kujipatia bidhaa hiyo muhimu.
Museveni
pia ametoa agizo kwa polisi kuwakamata wanasiasa watakaotoa misaada ya
chakula kwa jamii na kushtakiwa kwa ''jaribio la mauaji ''
Uganda kufikia sasa imethibitisha kuwa na wagonjwa 33 wa corona na maafisa wanatarajia idadi hiyo kuongezeka.
Magari
binafsi yatazuiwa kuingia barabarani baada ya maelekezo ya awali kutaka
magari kubeba abiria watatu pekee kukiukwa, na baadhi ya watu kutumia
magari binafsi kuwasafirisha wengine na kuongeza hatari ya kusambaa kwa
virusi hivyo.
-BBC
No comments:
Post a Comment