Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb)
akimfafanulia jambo Mratibu Mkazi wa Shughuli za Umoja wa Mataifa (UN)
Bw. Zlatan Milisic katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb)
akiisoma hati ya utambulisho mara baada ya kuipokea kutoka kwa Mratibu
Mkazi wa Shughuli za Umoja wa Mataifa (UN) Bw. Zlatan Milisic katika
Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) Bw. Antonio
Canhandula akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) kabla ya kukabidhi hati ya
utambulisho katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb)
akipokea hati ya utambulisho kutoka kwa Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) Bw. Antonio
Canhandula katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
…………………………………………………………………………………………………..
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb)
amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Mratibu Mkazi wa Shughuli za
Umoja wa Mataifa (UN) Bw. Zlatan Milisic Pamoja na Mwakilishi Mkazi wa
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) Bw.
Antonio Canhandula Jijini Dar es Salaam.
Waziri Kabudi amewaeleza Bw.
Milisic na Bw. Canhandula kuwa UN pamoja na UNHCR zimekuwa na mchango
mkubwa kwa kuiunga mkono Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
katika kukuza maendeleo pamoja na zile za kushughulikia masuala ya
wakimbizi.
“Kwa ujumla UN imekuwa ikisaidia
Tanzania kufanikisha agenda zake za maendeleo endelevu ya kijamii, na
kiuchumi hivyo Serikali itaendelea kuhakikisha inaendeleza uhusiano
huu,” Amesema Prof. Kabudi.
Kwa upande wake Mratibu Mkazi wa
Shughuli za Umoja wa Mataifa nchini (UN) Bw. Milisic amesema kuwa
uhusiano wa UN na Serikali ya Tanzania ni wa muda mrefu na hivyo ni
jukumu la UN kuhakikisha inaimarisha uhusiano huo na kuuboresha.
“Ni matumaini yangu kuwa uhusiano
huu tutauboresha vizuri na kuimarisha kwa maslahi mapana na maendeleo
endelevu ya taifa la Tanzania,” Amesema Bw. Milisic
Nae Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) Bw. Canhandula
amesema wanatambua mchango mkubwa ambao Tanzania imekuwa ikiutoa
kuhakikisha inaimarisha ulinzi wa maeneo ya wakimbizi ili wananchi wa
maeneo hayo waendelee kuishi kwa amani na utulivu pamoja na kupatiwa
mahitaji muhimu kama vile malazi na mavazi.
“Kwa kweli UNHCR tunafurahishwa na
jinsi Serikali ya Tanzania ambavyo imekuwa ikipokea wakimbizi na
kuwapatia baadhi ya mahitaji muhimu……tunaomba tuendeleze ushirikiano huu
kwa maendeleo yetu,” Amesema Bw. Canhandula.
No comments:
Post a Comment