Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumza wakati wa Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya
Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing linalofanyika
katika Ukumbi wa Hyatt Regency Hotel Jijini Dar es salaam. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
amewataka Wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za
Uongozi ikiwemo Udiwani na Ubunge katika Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka
2020.
Mhe.
Samia ametoa wito huo leo Jumatano Machi 4,2020 wakati akifungua
Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na
Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing linalofanyika katika Ukumbi wa
Hyatt Regency Hotel Jijini Dar es salaam.
Alisema
Mwaka 2020 ni mwaka wa uchaguzi hivyo ni vyema wanawake wakajitokeza
kuwania nafasi za uongozi huku akiwataka wanawake kuacha tabia ya
kubezana pale mwenzao anapojitokeza kugombea nafasi za uongozi.
“Huu ni mwaka wa uchaguzi,Wanawake tujitokeze katika
majimbo,tujitokeze kwa wingi katika nafasi za udiwani na kisha tujaze
kwa wingi fomu za viti maalumu. Tuhamasishe wanawake wajitokeze kugombea
nafasi za uongozi”,alisema.
“Wanawake ni Jeshi kubwa katika kuleta usawa lakini cha kushangaza
Mwanamke ndiyo wa kwanza kumponda mwenzie. Haya tuyaache,Ukiona mwanamke
mwenzio kachukua fomu ya kugombea msaidie siyo kumponda.Mimi mwenyewe
nimefikia hatua hii baada ya kushikwa mkono”,aliongeza.
Aliwaasa wanawake kushikamana kuiomba jamii kwa kuwashika mkono wanawake
wenye sifa za kuwa viongozi ili kuhakikisha idadi ya wanawake katika
meza za maamuzi inaongezeka hatimaye kufikia usawa wa kijinsia.
Alisema kuhusu suala la ushiriki wa wanawake katika meza ya maamuzi
serikali imechukua hatua kadhaa ili kuondoa vizingiti vinavyowazuia
wanawake wasishiriki kikamilifu katika meza ya maamuzi.
“Changamoto iliyopo ni uchache wa wanawake wenye uwezo wa kugombea
nafasi mbalimbali iwe kwenye uongozi wa kisiasa,biashara,asasi za kiraia
na sekta binafsi. Ni jukumu letu kama watetezi wa haki za wanawake
kushawishi wanawake wenye uwezo kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi
mbalimbali katika Nyanja tofauti”,alisema.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika lisilo la kiserikali la Women Fund
Tanzania (WFT) Prof. Ruth Meena Prof. Meena kutoka WFT,alisema licha ya
wanawake kuwa nguzo kuu ya Maendeleo katika kukuza uchumi wa nchi bado
wanabeba mzigo mkubwa wa kulea na kuendeleza kizazi cha taifa bila
nyenzo wezeshi katika kaya na jamii zao hali inayosababisha umaskini na
ufukara wa dunia kuendelea kubeba sura ya mwanamke na msichana.
Prof. Meena kutoka WFT inayofanya shughuli za utetezi wa haki za
wanawake na ujenzi wa tapo ya wanawake Tanzania,alisema pamoja na
ongezeko la wanawake na wasichana katika uongozi na meza za maamuzi
lakini bado ushiriki wao katika katika meza hizo za maamuzi haupo sawia
katika Nyanja zote za kisiasa,kiuchumi na hata ki – ustawi wa jamii.
“Pamoja na jitihada mbalimbali zinazofanyika kuleta mabadiliko kwenye
sera na sheria za nchi,bado kuna mifumo kandamizi na ya kiubaguzi katika
mifumo hi, hivyo kuna umuhimu wa uwajibikaji zaidi kwenye kubomoa
mifumo kandamizi hususani mfume dume”,alisema.
Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na
Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing likiongozwa na Kauli mbiu ya
''Uwajibikaji wa uongozi kwenye kujenga kizazi cha usawa wa jinsia''
limeandaliwa na Mtandao wa Wanawake na katiba, Uchaguzi na Uongozi kwa
ufadhili wa Women Fund Tanzania, Global Affairs Canada, Embassy of
Ireland, High Commission of Canada na WiLDAF.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akizungumza wakati wa Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea
Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing
linalofanyika katika Ukumbi wa Hyatt Regency Hotel Jijini Dar es
salaam. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akiwahamasisha wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za
uongozi katika Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2020.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika lisilo la kiserikali la Women Fund
Tanzania (WFT) linalofanya shughuli za utetezi wa haki za wanawake na
ujenzi wa tapo ya wanawake Tanzania, Prof. Ruth Meena akizungumza wakati
wa Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na
Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing.
Mwenyekiti wa Bodi ya WFT, Prof. Ruth Meena akizungumza wakati wa
Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na
Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing.
Mkurugenzi wa Women Fund Tanzania, Mary Rusimbi akizungumza wakati wa Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing.
Mkurugenzi wa Women Fund Tanzania, Mary Rusimbi akizungumza wakati wa Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi
akizungumza wakati wa majadiliano kwenye Kongamano la Kuadhimisha na
Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa
Beijing.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Msichana Initiative Rebeca Gyumi
akizungumza wakati wa majadiliano kwenye Kongamano la Kuadhimisha na
Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa
Beijing.
Wadau wa haki za wanawake wakiwa kwenye kwenye Kongamano la Kuadhimisha
na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa
Beijing.
Wadau
wa haki za wanawake wakiwa kwenye Kongamano la Kuadhimisha na
Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa
Beijing.
Mkurugenzi
Mtendaji wa shirika la Door of Hope Tanzania,Clemence Mwombeki
akichangia hoja kwenye Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya
Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing.
MwanaMtandao Asseny Muro akichangia hoja kwenye Kongamano la Kuadhimisha
na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano
wa Beijing.
Meneja Miradi wa shirika la Young Women Leadership (YWL) mkoani Shinyanga Veronica Massawe akichangia hoja kwenye Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing.
Mkurugenzi wa Women Fund Tanzania, Mary Rusimbi akichangia hoja kwenye Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing.
Wadau
wa haki za wanawake wakiwa kwenye kwenye Kongamano la Kuadhimisha na
Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa
Beijing.
Wadau
wa haki za wanawake wakiwa kwenye kwenye Kongamano la Kuadhimisha na
Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa
Beijing.
Wadau
wa haki za wanawake wakiwa kwenye kwenye Kongamano la Kuadhimisha na
Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa
Beijing.
Wadau
wa haki za wanawake wakiwa kwenye kwenye Kongamano la Kuadhimisha na
Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa
Beijing.
Wadau
wa haki za wanawake wakiwa kwenye kwenye Kongamano la Kuadhimisha na
Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa
Beijing.
Wadau
wa haki za wanawake wakiwa kwenye kwenye Kongamano la Kuadhimisha na
Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa
Beijing.
Wadau
wa haki za wanawake wakiwa kwenye kwenye Kongamano la Kuadhimisha na
Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa
Beijing.
Wadau
wa haki za wanawake wakiwa kwenye kwenye Kongamano la Kuadhimisha na
Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa
Beijing.
Wadau
wa haki za wanawake wakiwa kwenye kwenye Kongamano la Kuadhimisha na
Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa
Beijing.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akipiga picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano la Kuadhimisha na
Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa
Beijing linalofanyika katika Ukumbi wa Hyatt Regency Hotel Jijini Dar es
salaam.
Wajumbe
wa kamati ya Maandalizi ya Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea
Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing
wakipiga picha ya kumbukumbu.
Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
No comments:
Post a Comment