Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa
Mara Jerome Kiwia akimuonesha Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo
ya Makazi Dkt Angeline Mabula sehemu ya Ofisi mpya za Ardhi mkoa wa
Mara wakati Naibu Waziri alipokwenda kuzikagua ofisi hizo mkoani Mara
jana. Kulia kwa Naibu Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Musoma Dkt Vincent
Naano Anney.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akikagua ofisi mpya za Ardhi
mkoa wa Mara wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya
ardhi mkoani Mara jana. Kulia kwa Naibu Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya
Musoma Dkt Vincent Naano Anney na Kulia ni Kamishna Msaidizi wa Ardhi
mkoa wa Mara Jerome Kiwia.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akioneshwa sehemu kitakachowekwa
kibao cha kuitambulisha ofisi mpya za Ardhi mkoa wa Mara na Kamishna
Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Mara Jerome Kiwia alipofanya ziara ya kukagua
utendaji kazi wa sekta ya ardhi mkoani Mara jana (PICHA NA MUNIR
SHEMWETA WIZARA YA ARDHI)
………………………………………………………………………………………………..
Na Munir Shemweta, WANMM MUSOMA
Naibu Waziri wa
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amesema wizara
yake itaipatia ofisi ya ardhi mkoa wa Mara vifaa vya upimaji ili viweze
kutumiwa na
halmashauri za mkoa huo kwa lengo la kuongeza kasi ya
upimaji.
Dkt Mabula alitoa
kauli hiyo jana wilayani Musoma mkoa wa Mara alipokwenda kukagua ofisi
mpya ya ardhi ya mkoa Mara ikiwa ni jitihada za wizara ya ardhi kusogeza
huduma za ardhi kwa wananchi.
Awali huduma za
ardhi zilikuwa zikitolewa na ofisi za Mkamishna Wasaidizi wa Kanda
ambapo kanda moja ilikuwa ikihudumia zaidi ya mikoa miwili jambo
lililokuwa likiwapa usumbufu wamiliki wa ardhi kwenda umbali mrefu
kuifuata huduma hiyo.
Alisema, baada ya
wizara yake kuanzisha ofisi za mikao sasa wananchi watapata huduma za
ardhi katika mikoa husika na migogoro ya ardhi sasa itapatiwa ufumbuzi
kupitia wataalamu watakaokuwa katika mikoa hiyo.
Alibainisha kuwa,
katika jitihada za kuongeza kasi ya upimaji maeneo mbalimbali ofisi za
mikoa zitapatiwa vifaa vya upimaji ili visaidie halmashauri kupanga,
kupima na kumilikisha ardhi na kusisitiza vifaa hivyo vitatolewa bure na
aliwataka wakurugenzi wa halmashauri kushirikiana na ofisi za ardhi za
mikoa.
Kwa mujibu wa
Naibu Waziri Mabula, Wizara yake imeamua kubeba jukumu la kutoa vifaa
vya upimaji ili kuongeza kasi ya upimaji ingawa jukumu hilio linapaswa
kufanywa na halmashauri kwa kuwa ndizo zenye mamlaka za upangaji miji
katika maeneo.
Dkt Mabula
amesikitishwa na kiasi kidogo kinachotengwa na halmashauri kwa ajili ya
kazi za kupanga, kupima na kumilikisha ardhi ambapo alitolea mfano wa
halmasahauri ya Musoma kutenga milioni 30 kwa kazi mbalimbali za sekta
ya kiasi alichokieleza kuwa kidogo.
‘’Milioni 10 au
15 utapima viwanja vingapi? Halmashauri hazijaipa kipaumbele sekta ya
ardhi ndiyo maana malalamiko yanakuwa mengi, muongeze bajeti za
upimaji’’ alisema Dkt Mabula
Hata hivyo,
ameishauri halmashauri ya wilaya ya Musoma kuwatumia wataalamu wake kwa
kuandika andiko ili kupatiwa mkopo usio na riba unaotokewa na wizara kwa
ajili ya shughuli za umilikishaji ardhi ambapo alisema katika kipindi
caha bajeti ijayo wizara inatarajia kupata bilioni saba kwa ajili ya
kuzikopesha almashauri.
Kwa upande wake
Mkuu wa wilaya ya Musoma Dkt Vincent Naano Anney aliipongeza wizara ya
ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa uamuzi wake wa kuanzisha ofisi
za mikoa na kueleza kuwa uamuzi huo utaleta nafuu kwa wananchi wa mara
katika kupata huduma za ardjhi ambapo awali iliwalazimu kusagiri hadi
Simuiyu kupata huduma hiyo.
No comments:
Post a Comment