Mwakilishi wa Katibu MkuuIdara Kuu
ya Maendeleo ya Jamii Bi. Imelda Kamugisha akizungumza na wananchi wa
mkoa wa Shinyanga wakati wa mapokezi ya msafara wa kijinsia ulifika
mkoani humo kwa lengo la kutoa elimu ya kupambana na vitendo vya ukatili
wa kijinsia.
Wasanii Shetta na G nako
wakitumbuiza katika Eneo la nguzo nane Mkoani Shinyanga wakati Msafara
wa kijinsia unaolenga kutoa elimu ya mapambano dhidi ya vitendo vya
kikatili uliposimama mkoani hapo.
Baadhi ya wasaidizi wa kisheria
wakitoa msaada wa kisheria kwa waanchi wa mkoa wa
Shinyangawaliojitokeza kuupokea msafara wa kijinsia unaolenga kutoa
elimu kwa wananchi kuhusu madhara ya vitendo hivyo.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
*****************************
Na Mwandishi Wetu Tabora
Timu ya Msafara
wa kijinsia unaolenga kutoa elimu juu ya madhara ya ukatili wa
kijinsia
umefakiwa kumpa ubalozi na kumjuwezeshakijana .. baiskeli itakayomsadia
kujikwamua kuchumi na kuwa mfano kwa vijana na jamii katika mapambano
dhidi ya vitendo vya kikatii mkoani Shinyanga.
Hayo yamefanyika
jana mkoani humo wakatiwa mapokezi ya Msafara wa Kijinsia kutokomeza
ukatili unaolenga kutoa elimu kwa jamii kuhusu madhara ya kufanya
vitendo vya ukatili wa kijinsia kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake
Duniani yatakayofanyika Kitaifa Simiyu Machi 08, 2020.
Akizungumza kwa
niaba ya Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jmaii, Afisa Maendeleo ya
Jmaii Mkuu Bi. Imelda Kmaugisha amesema kuwa Mkoa wa Shinyanga ni
miongoni mwa mikoa inayoongoza kwa wanafunzi na watoto wadogo wa kike
kupata mimba nakuopewa katika umri mdogo.
“Hapa Shinyana
kuna vitendo sana vya watoto wa kike na wananfunzi kupewa mimba wakiwa
bado wadogo na kuolewa pia hili sio swa naomba tulikemee kwa nguvu moja”
alisema
Aidha amwataka
vijana hasa waendesha baiskeli, bodaboda na bajaji kuwa mabalozi wazuri
wa kutoa taarifa katka vyombo vya usalama mara waonapo vitendo hivyo
vikitokea kwani watakuwa wameisadia jamii kuondokana na vitendo hivyo
vinavyokatisha ndoto hasa za watoto wa kike nchini.
“Wanaofanya
vitendo hivi ni watu wa karibu na familia zetu wanawapa mimba watoto
wetu tunanyamaza kisa ndugu wengine wazazi na walezi wanaowaozesha
watoto wakiwa wadogo hili sio sawa kabisa” alisema
Akitoa shukrani
zake mara baada ya kupewa ubalozi na baiskeli kwa ajili ya biashara
Martin Christopher Matiku amishauri jamii ya mkoa wa Shinyanga kuwa pia
mabalozi wazuri wa kuhakikisha wanakemea vitendo vya ukatili wa kijisia
katika maeneo yao ili kuweza kuunga mkono juhudi za Serikali katika
kuhakikisha vitendo vya ukatili wa kijinsia vinatokomea.
“Naushukuru huu
Msafara wa Twende Pamoja naahidi nitakuwa Balozi mzuri na nitasaidiz
kutoa elimu juu ya adhara ya vitendo vya ukatili naamini itasaidia
kuokoa watoto wa kikena kiume na wanawake katika madhara haya” aliseNaye
Mtoa Huduma za Kisheria mkoa wa Shinyanga Anna Kadaso Mtao amesema
kuwa kesi nyingi zinazopokelewa katika madawati hayo ni za vitendo vya
ukatili wa kijinsia hasa vipigo unynyasaji wa wanawake katika mirathi na
kesi za wanaume wakinyanyaswa pia zipo ingawa bado sio nyingi
zinztolewa taarifa,
Msafara wa
kijinsia kutokomeza ukatili wa kijinsia upo katika mzunguko ulioanzia
mkoa wa Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa, Tabora na umefika mkoani
Shinyanga kuelekea Shinyanga na utapokelewa mkoani Simiyu kuelekea
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
No comments:
Post a Comment