Katibu Mkuu wa Sekta ya Uchukuzi,
Dkt. Leonard Chamuriho, akitoa maelekezo kwa Uongozi wa Kampuni ya
Huduma za Meli (MSCL) wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa meli mpya,
chelezo na Ukarabati wa Meli ya MV Victoria jijini Mwanza, Mwishoni mwa
wiki. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, Eric Hamissi.
Katibu Mkuu wa Sekta ya Uchukuzi,
Dkt. Leonard Chamuriho, akitoa maelekezo kwa Uongozi wa Kampuni ya KTMI
ya Korea Kusini inayofanya ukarabati wa meli Meli ya MV Victoria jijini
Mwanza, Mwishoni mwa wiki, wakati alipotembelea maendeleo ya ujenzi
wake.
Muonekano wa Chelezo inayojengwa katika bandari ya Mwanza South ambayo ujenzi wake umefikia asilimia 96. Kukamilika kwa chelezo kutarahisisha matengenezo ya meli katika Ziwa Victoria.
Katibu Mkuu wa Sekta ya Uchukuzi,
Dkt. Leonard Chamuriho, akimsikiliza Muwakilishi wa Kampuni ya KTMI ya
Korea Kusini, inayojenga meli mpya katika bandari ya Mwanza South
wakati akimweleza hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa meli, wakati Katibu
Mkuu huyo alipotembelea maendeleo ya ujenzi wake mwishoni mwa wiki.

Muonekano wa meli ya MV Victoria
mara baada ya ukabati mkubwa ambao mpaka sasa umefikia asilimia zaidi ya
96. Meli hiyo ina uwezo wa kubeba abiria 1,200 na mzigo wa tani 200.
No comments:
Post a Comment