Jaji Kiongozi
wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Eliezer Feleshi (katikati) akikagua
leo ujenzi wa jengo la Kituo cha Mahakama Jumuishi cha Utoaji Haki
(IJC) kilichopo Kinondoni. Kituo hicho kinajumuisha Mahakama Kuu,
Mahakama ya Hakimu Mkazi na Mahakama ya Wilaya, Mahakama ya Mahakama
Mwanzo, zikiwemo ofisi za wadau wote wa Mahakama.
Hakimu Mkuu Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo Kariakoo akitoa (kushoto)taarifa ya utendaji wa Mahakama hiyo kwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Eliezer Feleshi( ambaye hayupo pichani).

Jaji Kiongozi
wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Eliezer Feleshi (kulia) na Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam( kushoto) (katikati)
akinawa mikono mara ikiwa ni hatua ya kupambana na maambukizi ya
virusi vinavyosababisha vya ugonjwa wa Corona baada ya kuwasili leo
katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni na Mahakama ya Wilaya
ya Kinondoni, Jijini Dar es Salaam. Jaji Kiongozi yuko katika ziara
maalum ya kikazi kwenye Mahakama Kuu ya Kanda ya Dar es Salaam.
Picha na Magreth Kinabo- Mahakama
*******************************
Na Magreth Kinabo- Mahakama
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya
Tanzania, Mhe. Eliezer Feleshi, amewataka Mahakimu
kusikiliza kesi za
jinai kwa mfululizo ili ya kuweza kupunguza msongamano wa mahabusu,
na kuepukana na maambukizi ya Virusi Corona.
Jaji Kiongozi alitoa agizo hilo
leo mara baada ya kutembelea mahakama mbalimbali za Mahakama Kuu Kanda
ya Dar es Salaam kwa ajili ya ukaguzi maalum.
“Anzeni kusikiliza kesi za jinia
mfululizo, itasaidia tusiwe na msongamano wa mahabusu, na wale
wanaostahili dhamana wapewe, hatua hii itatuwezesha kujikinga na
maambukizi ya virusi vya Corona, alisema Jaji Kiongozi.
Aidha Jaji Kiongozi
amewataka watumishi wa Mahakama kuendelea kuepukana na vitendo vya
rushwa na kuzingatia maadili ya kazi zao.
Dkt. Feleshi alizipongeza Mahakama za Mwanzo kutokuwa na mlundikano wa mashauri.
Jaji Kiongozi ameanza ziara ya
ukaguzi maalum katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ambayo
inatarajiwa kumalizika Aprili 3, mwaka huu.
Katika ziara hiyo Jaji Kiongozi
alikagua ujenzi wa ujenzi wa jengo la Kituo cha Mahakama Jumuishi
cha Utoaji Haki (IJC) kilichopo Kinondoni. . pia alikagua Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kivukoni, Mahakama ya Wilaya Kinondoni na Mahakama za
Mwanzo za Sinza, Kinondoni,Kaw. Kimara, Magomeni na Kariakoo.
No comments:
Post a Comment