
Waziri Mkuu – Kassim Majaliwa (wa
tatu kushoto) akipokea hundi ya Sh. Milioni 100 kwa ajili ya mapambano
dhidi ya ugonjwa wa Corona kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya NMB –
Ruth Zaipuna (wa nne kutoka kushoto) Kushoto ni Afisa Mkuu wa Wateja
Wakubwa wa Serikali wa NMB Alfred Shao na kulia ni Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto- Ummy Mwalimu.
Waziri Mkuu- Kassim Majaliwa akizungumza na uongozi wa Benki ya NMB.
………………………………………………………………………………………..
Kama mchango wa Benki ya NMB
katika kudhibiti na kupambana dhidi ya virusi vya Corona, Kaimu
Mkurugenzi wa Benki ya NMB-Ruth Zaipuna amekabidhi msaada wa kifedha
shilingi Milioni 100 kwa Mhe. Waziri Mkuu – Kassim Majaliwa mbele ya
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
– Ummy Mwalimu pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali. Makabidhiano
hayo yamefanyika mwishoni mwa wiki katika ofisi ya Waziri Mkuu-Dar es
Salaam.
Benki ya NMB ikiwa na maadhimio
sawa ya kuudhibiti ugonjwa huu, mchango huu utaisaidia serikali katika
mapambano dhidi ya virusi hivi.
Tunasisitizwa kuendelea kutumia njia stahiki kujikinga na maambukizi.
#TanzaniaBilaCoronaInawezekana
#JikingeMlindeMwenzio
No comments:
Post a Comment