Afisa Uendeshaji wa Mifuko hiyo, Bi. Kashinje Sekule Felician, akiwasilisha mada kuhusu Mifuko hiyo Machi 5, 2020.
Afisa Uendeshaji wa Mifuko hiyo, Bi. Kashinje Sekule Felician, akiwasilisha mada kuhusu Mifuko hiyo Machi 5, 2020.
Kutoka kushoto kwenda kulia, Bi. Vicky Msina, Meneja Msaidizi Uhusiano na Itifaki (BoT), Bi.Kashinje Sekule Felician, Afisa Uendeshaji wa Mifuko ya Udhamini ya BoT, Bi. Zalia Mbeo, Meneja Uhusiano na Itifaki BoT, Bw. Ganga Ben Mlipao, Meneja
Msaidizi, Dawati la
Kutatua Malalamiko ya wateja wa mabenki na taasisi za fedha, BoT na
Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki, BoT Bw. Augustino Hotey, wakiwa kwenye
semina hiyo.
Bi. Zalia Mbeo, Meneja Uhusiano na Itifaki BoT, akizungumza na wanasemina kuelezea malengo ya BoT kutoa elimu ya masuala ya Uchumi na Fedha kwa wanahabari
Bi.
Vicky Msina, Meneja Msaidizi Uhusiano na Itifaki BoT, akielezea uzoefu
wake kwa washiriki jinsi alivyokuwa akifanya kazi za uandishi wa habari.
Bi. Zalia Mbeo, Meneja Uhusiano na Itifaki BoT, akizungumza na wanasemina kuelezea malengo ya BoT kutoa elimu ya masuala ya Uchumi na Fedha kwa wanahabari
Baadhi ya washiriki wa semina wakiwa kwenye semina hiyo.
Baadhi ya washiriki wa semina wakiwa kwenye semina hiyo.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Arusha
BENKI
Kuu wa Tanzania BoT imeridhishwa na mafanikio waliyofikia wananfunzi wa
elimu ya juu waliosoma na wanaoendelea kusoma kupitia Mifuko ya udhamini inayosimamiwa na benki hiyo.
Benki Kuu ya Tanzania ilianzisha Mifuko ya Gilman
Rutihinda Trust Fund na Mwalimu
Nyerere Memorial Trust Fund ili
kutoa hamasa ya ufaulu kwa wanafunzi katika masomo ya Hidsabati na
Sayansi hususan wanafunzi wa kike kwa kutoa ufadhili huo (Scholarships) , Afisa
Uendeshaji wa Mifuko hiyo, Bi. Kashinje
Sekule Felician amewaambia waandishi wa habari wanaoshiriki semina ya
kuwajengea uwezo wa kuandika kwa usahihi habari Uchumi na Fedha kwenye
ukumbi wa BoT jijini Arusha leo Machi 5, 2020.
Amesema katika kutekeleza sera ya kuwajibika kwa jamii (Corporate Social Responsibility-CSR),
Benki Kuu ya Tanzania ilianzisha mifuko hiyo ili kutoa hamasa kwa wanafunzi wa Kitanzania kufanya
vizuri kwenye masomo ya Hisabati na Sayansi, hususan wanafunzi wa kike.
Akiwasilisha mada kuhusu Mifuko
ya udhamini inayosimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania, (BoT)
Bi.Kashinje alisema, wamekuwa wakiwafuatilia wanafunzi hao na kubaini
kuwa wamekuwa wakifanya vizuri kwenye masomo yao kila mwaka na wengi wao
tayari wamehitimu na kuajiriwa kwenye taasisi mbalimbali ikiwemo Benki
Kuu.
"Wengi wamefaulu kwenye daraja la kwanza na wachache sana daraja la
pili na tayari baadhi yao wanalitumikia taifa kwenye Nyanja mbalimbali, wengine
wamebaki kwenye vyuo hivyo walikosoma na kuajiriwa kama wahadhiri wasaidizi na
kwa jambo hili tinafarijika sana. “ Alisema Bi. Kashinje
Akitoa historia ya mifuko hiyo na lengo la kuanzishwa kwake, Bi Kashinje alisema Mfuko wa Gilman Rutihinda
Trust Fund ulianzishwa mwaka 1994 kama kumbukumbu ya aliyewahi kuwa Gavana wa BoT, Marehemu Gilman
Rutihinda na Mfuko mwingine ni wa Mwalimu Nyerere
Memorial Trust Fund ambao ni kumbukumbu ya Hayati Babab wa Taifa.
"Mfuko wa Gliman Rutihinda ulianza kutoa ufadhili mwaka 1995 na unatoa
ufadhili kwa wanafunzi wa Kitanzania wa Chuo Kikuu waliofaulu kwa daraja la juu kabisa kwenye
masomo ya Uchumi na Fedha na wana umri usiozidi miaka 35 na
wanahitaji kuchukua Shahada ya Pili.
“Njia tunayotumia kuwapata walengwa ni pamoja na matangazo
kwenye radio, magazeti, televisheni na tovuti ya BoT.
Aidha Mfuko wa Mwalimu Nyerere unatoa ufaulu kwa wanafunzi
waliohitimu mkidato cha sita na kupata alama za juu kabisa katika masomo ya
Hisabati na Sayansi.
Alisema
mwaka 1995 Mfuko ulianza kufadhili wanafunzi wawili lakini idadi
imezidi kukua na sasa kuna jumla ya wanafuzni 37 na kati ya hao 33
wamekwisha kamilisha kozi
zao na wengine tayari wameajiriwa.
Aidha Mfuko wa Mwalimu Nyerere ulianza mnamo mwaka 2009 na ulianza
kutoa ufadhili mwaka 2013 ambapo nia ni kuongeza hamasa na ufaulu kwa wanafunzi
wa kike katika masomo ya Sayansi na Hisabati.
Aidha Shahada ya kwanza asilimia 50 ya ufadhili unaende kwa
wanafunzi wa kike ambaye ni raia wa Tanzania na awe na ufaulu wa juu Daraja la
Kwanza katika masomo ya Hisabati na Sayansi na awe amepata udahili kwenye vyuo
vikuu vya hapa nchini.
“Utaratibu wa kuwapata wanafunzi hawa huwa tunawailiana na
Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) ambapo hutuchagulia wananfunzi wenye vigezo
hivyo.” Alifafanua.
Ufadhili unahusisha fedha za ada, kujikimu, mafunzo kwa
vitendo na computer mpakato
Hadi sasa watanzania 46 wamenufaika na kati ya hao 32 ni
wanawake na 12 ni wanaume. Alisema Bi.Kashinje.
No comments:
Post a Comment