Sehemu ya Maafisa na Akari wa Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji wa Kiwanja cha Ndege Jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya
siku tano ya kuwajengea uwezo. Mafunzo hayo yanafanyika katika Ofisi za Jeshi
la Zimamoto na Uokoaji Kiwanja cha Ndege jijini Dodoma na kuratibiwa na Mamlaka
ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA) kwa kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji.
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Dodoma
Kamishna Msaidizi wa Zimamoto na Uokoaji (ACF) Gilbert Mvungi, akizungumza na
Maafisa na Akari wa Jeshi hilo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tano ya
kuwajengea uwezo Maafisa na Akari wa Kiwanja cha Ndege Jijini Dodoma. Mafunzo
hayo yanafanyika katika Ofisi za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kiwanja cha Ndege
jijini Dodoma na kuratibiwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA) kwa
kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Meneja wa Uwanja wa Ndege Jijini Dodoma Bertha Bankwa
(wapili kulia), akimshukuru Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa
Dodoma Kamishna Msaidizi wa Zimamoto na Uokoaji (ACF) Gilbert Mvungi (watatu
kulia), Kamishna Msaidizi wa Jeshi hilo ambaye ni Mkuu wa Zimamoto na Uokoaji
Viwanja vya Ndege nchini (ACF) Bakari Mrisho (watatu kushoto), Kamishna
Msaidizi Mstaafu wa Jeshi hilo (ACF) Christom Manyologa (kulia) kwa kuona haja
ya kuandaa mafunzo hayo kwani yataongeza ufanisi katika utendaji kazi kwa
Maafisa na Askari hao. Mafunzo hayo yanafanyika katika Ofisi za Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji Kiwanja cha Ndege jijini Dodoma na kuratibiwa na Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege nchini (TAA) kwa kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji.
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Dodoma
Kamishna Msaidizi wa Zimamoto na Uokoaji (ACF) Gilbert Mvungi (watatu kulia
waliokaa), Kamishna Msaidizi wa Zimamoto na Uokoaji ambaye ni Mkuu wa Zimamoto
Viwanja vya Ndege nchini (ACF) Bakari Mrisho (watatu kushoto waliokaa), Meneja
Uwanja wa Ndege Jijini Dodoma Bertha Bankwa (wapili kulia waliokaa), Kamishna
Msaidizi Mstaafu wa Jeshi hilo (ACF) Christom Manyologa (kushoto), Mratibu wa
mafunzo Uwanja wa Ndege Dodoma Swalha Soka (wapili kushoto waliokaa), Mkuu wa
Kituo cha Zimamoto na Uokoaji Uwanja wa Ndege Dodoma Liberatus Monella (kulia),
wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa na Askari wa Jeshi hilo, baada ya
Kamanda wa Mkoa wa Dodoma wa Jeshi hilo, kufungua mafunzo ya siku tano ya
kuwajengea uwezo Maafisa na Akari wa Kiwanja cha Ndege Jijini Dodoma.
Mafunzo hayo yanafanyika katika Ofisi za Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji Kiwanja cha Ndege jijini Dodoma na kuratibiwa na Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege nchini (TAA) kwa kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji.
Aidha imeelezwa kuwa mafunzo hayo yataendelea kwa siku
tano mfululizo, na zaidi ya Maafisa na Askari 30 watanufaika na mafunzo hayo
pia yataendelea kwa Mikoa mingine kote nchini
Taarifa ya Jeshi hilo imeeleza kuwa dhumuni la mafunzo
hayo kuhakikisha Maafisa na Askari wote wanaohuduma Viwanja vya Ndege kote nchini
wanapatiwa mafunzo ya aina hiyo kwa awamu hasa katika kipindi hiki tunapoelekea
Tanzania ya Uchumi wa kati unaotegemea Viwanda.
No comments:
Post a Comment